Poleni sana Simba, tukubali anaejua akidhamiria lazima ashinde

Poleni sana Simba, tukubali anaejua akidhamiria lazima ashinde

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Ni kweli huko nyuma Simba aliweza kuwafunga Al Ahly na timu zingine kubwa. Pamoja na kwamba Simba alizifunga hizo timu, ilikuwa ni kujidanganya kudhani tayari Simba yupo nao level moja.

Kwa mfano Simba imewahi fungwa na kutolewa mara mbili kombe la Azam Confederation na Green warrior,na Mashujaa km sijakosea.Haikumaanisha Greenwarrior alifikia level za Simba. Naamini Simba alitolewa na hizi timu kwa kuzembea na "too much underestimation"kuanzia upangaji wa kikosi hadi kujituma uwanjani. Inawezekana pia kina Al ahly waliichukulia poa Simba na kuishia kuaibika. Sasa hicho kimewaamsha ma- "Giant" wengine kwamba wanapokuja kwa Mkapa hawaji tena kulemba mwandiko.Wanajua wakizembea kidogo wataaibika.

Ukiangalia mchezo wa jana unaona kabisa Raja Casablanca walikuja kutafta matokeo.Unawaona kabisa wakipoteza mpira wote wanageuka kuwa wakabaji huku wakiziba mianya vizuri. Hata wakiamua kushambulia wanashambulia kwa nguvu na mbinu za uhakika. Simba walipoteana kila idara japokuwa wengi wanamtupia lawana Sawadogo huku wakisahau hata kina Chama,Boko,Saido,Sakho hakuna cha maana walichokifanya. Aishi mwenyewe na mabeki wake wote walikuwa vichochoro.

Unapokuwa na wachezaji wa viwango vya juu halafu wakaamua kucheza mpira mara nyingi matokeo yake huwa "Dhahama," km kilichowakuta Simba jana. Tukubali,pamoja na heshima ambayo Simba wametuheshimisha Watanzania kwa miaka kadhaa bado hatujafikia viwango vya wenzetu,tuendelee kuiga na kujifunza kutoka kwao. Hasa kuwekeza kwenye wachezaji bora. Tulichokiona jana ni tofauti kati ya Hamasa( Simba) VS Ubora (Raja Casablanca).

Kwasasa Simba na Yanga zina wachezaji wa kuweza kutupeleka kwenye makundi na nadra robo fainali. Ila Kuingia nusu na hata fainali tutahitaji vilabu kuwa "Giant" kiuchumi kuweza kusajili "best players in the continent." na sio "players" ambao wanakuja kula "pension" au kuboresha viwango vyao kutokana na majeraha ya muda mrefu.

Lion King never loose,he either win or learn new experiences.

images%20(43).jpg
 
Pitso mosimane kipindi yupo mamelods alisema vilabu vya kaskazini vimeizidi mamelods kwa kila kitu kwanzia bajeti Hadi aina ya sajili wanazofanya.

Njia pekee ya kupambana navyo ni kuhakikisha una kua na wachezaji wenye quality kubwa na kupewa mbinu sahihi za makocha.

Leo mamelods wana kikosi chenye 98% wazawa wa south na wana quality ya kupambana na timu yoyote Africa
 
Back
Top Bottom