Mpira wa leo kati ya Wekundu wa Msimbazi na Nkana Red Devils ulikuwa mkali sana japo Simba wamefungwa goli 2-1wakiwa na faida ya goli la ugenini. Mnatakiwa mjipange sana kwa ajili ya mechi ya nyumbani. Simba inaweza kujifariji kuwa hapa ni nyumbani LAKINI Nkana ni timu nzuri na hata asilimia ya kumiliki mpira waliwazidi Simba.Nadhani mlimuona Kessy anavyokokota mpira japo mlimuona hafai. Marudio ni baada ya wiki mbili msije mkarudi tena kwenye ligi mkiwa mnashika namba tatu. Ninawatia kila la kheri wewe Wekundu wa Msimbazi.