Poleni Wabongo kwa kipigo cha Msudani

Poleni Wabongo kwa kipigo cha Msudani

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kaimu kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Juma Mgunda amewaomba radhi mashabiki wa soka na Watanzania kwa ujumla baada ya kupoteza mchezo wa nyumbani jana dhidi ya Sudan.

PIC11.jpg

Mchezo wa Taifa Stars na Sudan katika Uwanja wa Taifa
Katika mchezo huo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani 'CHAN' uliofanyika jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Taifa Stars imefungwa bao 1-0, bao la Sudan likifungwa katika dakika ya 61 na Yassir.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha Juma Mgunda amesema kuwa wanafahamu Watanzania wanahitaji furaha na walikuwa na mategemeo makubwa katika mchezo huo lakini mpira una matokeo tofauti.
"Nichukue nafasi hii kuwatakeni radhi Watanzania wote kwa ujumla kutokana na matokeo tuliyoyapata, hii ni sehemu ya mchezo na tumeona kilichotokea, tulijitahidi kutafuta ushindi lakini haikuwa hivyo", amesema.
"Kila mmoja ameona mchezo tulivyocheza, tutakwenda kufanyia kazi mapungufu yaliyotokea. Nirudie tena kuwaomba radhi, hatukupenda kuwaudhi lakini muendelee kutuombea, msichoke", ameongeza Mgunda.
Mchezo wa marudiano unatarajia kupigwa Oktoba 18, 2019 katika uwanja ambao si wa nchi ya Sudan kutokana na hali ya nchi hiyo kutokuwa sawa.

Punguza shobo,
Unaacha kuipa timu yenu pole unaangaika na Taifa stars ambayo bado ina nafasi tena iliwafunga harambee stars 4 =1 na tukawafungasha virago kabisa[emoji23][emoji23][emoji23]
Ona tena juzi timu yenu ilivyo tia aibu.

Tukishinda pia uwe unaandika thread za kutupongeza tusiishi kwa kuviziana.Tunaenda kuwapiga kwao kama tulivyowafanya majirani.ASANTE
 
Tukishinda pia uwe unaandika thread za kutupongeza tusiishi kwa kuviziana.Tunaenda kuwapiga kwao kama tulivyowafanya majirani.ASANTE

Kwao huko hamuendi, itabidi ichaguliwe nchi nyingine mkashindanie huko, maana kwao Sudani hakukaliki full vurugu, mkibahatika kuwashindia kwao ndio mtajua mwarabu hatanii.
 
Kwao huko hamuendi, itabidi ichaguliwe nchi nyingine mkashindanie huko, maana kwao Sudani hakukaliki full vurugu, mkibahatika kuwashindia kwao ndio mtajua mwarabu hatanii.
UOGA NI ADUI WA MWAFRICA acha uonga[emoji23][emoji23][emoji23]

Sisi ni wanaume kamili hatuogopi pia tupo tiyari kwa lolote

Tuliza matako[emoji23][emoji23][emoji23]
 
UOGA NI ADUI WA MWAFRICA acha uonga[emoji23][emoji23][emoji23]

Sisi ni wanaume kamili hatuogopi pia tupo tiyari kwa lolote

Tuliza matako[emoji23][emoji23][emoji23]
Umesoma taarifa na kuzielewa kweli....

Mchezo wa marudiano unatarajia kupigwa Oktoba 18, 2019 katika uwanja ambao si wa nchi ya Sudan kutokana na hali ya nchi hiyo kutokuwa sawa.
 
Umesoma taarifa na kuzielewa kweli....

Mchezo wa marudiano unatarajia kupigwa Oktoba 18, 2019 katika uwanja ambao si wa nchi ya Sudan kutokana na hali ya nchi hiyo kutokuwa sawa.
Tutacheza hivyo hivyo sisi ndo mabaharia
 
Back
Top Bottom