MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Baada ya kutazama video nzima ya Polepole ya dakika 59 nimeona niandike huu uzi ili kuweka mambo sawa kwa facts tupu. Huu uzi ndo utakuwa msimamo wa JF nzima dhidi ya vioja vya Polepole. Nimejitahidi kumpuuza ila naona anakoelekea sio pazuri kwa afya yake ya akili ndo maana nimeona nimsaidie yeye na nyumbu zinazomuamini kwa kuandika huu uzi. Polepole ni active member wa JF hivyo atasoma huu uzi.
Kwenye video yake Polepole kaanza kwa kudai kuwa rais mstaafu JK alikuwa akimchukia na kumshauri hayati Magufuli amtimue yeye Polepole kwenye nafasi yake. Ni ngumu sana kuamini hili ila hata kama mimi ningekuwa na nafasi kama ya JK kuongea na Rais moja kwa moja ningemshauri atumbue Polepole haraka sana. Sababu kuu ni kuwa alikuwa mwenezi fisadi aliyetumia cheo chake kihuni kudhulumu haki za wengi.
Polepole akiwa mwenezi ndo tuliona manunuzi ya viongozi wa upinzani kama ng'ombe mnadani kwa kile kilichoitwa kuunga mkono juhudi za JPM. Polepole ndo kama alikuwa kapewa hii tenda. Kimsingi alikuwa katibu mwenezi aliyefanya kazi zake kihuni mno na adui wa demokrasia. Pia kwa wale wasiojua ni kuwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020 Polepole alikusanya rushwa ya mamilioni kwa waliokuwa wanautaka ubunge. Alikuwa akichukua hadi 400m kwa kichwa. Kama ni kweli JK alishauri Polepole apigwe chini alifanya la maana sana ili kuinusuru demokrasia.
Kwamba JPM alifariki baada ya kutoka kufungua kiwanda cha Rostam ni hoja ya kijinga mno. Siku ikifika kila mmoja wetu atafariki kwa namna yake. Mwengine atafariki baada ya kutoka kanisani au msikitini, mwingine atafariki baada ya kutoka gest house nk. Isitoshe JPM aliendelea na shughuli zake nyingine mara baada ya kutoka Morogoro. Alichofanya Polepole ni uhuni wa kutamka kitu kumchafua Rostam.
Kwamba yeye ndo alikuwa akipewa taarifa za siri za watu kutaka kumuua Rais JPM ni jambo jingine linaloashiria kuwa Polepole alikuwa mnafiki mno kwa JPM. Ni wazi alikuwa kitu kimoja na hao waliokuwa na mipango miovu ila akawa anafanya ujanja wa kujisafisha mapema kabla kitu kibaya hakijatokea. Kuna wahuni wengine huweza hata kuua na kuwa wa kwanza kutoa taarifa polisi. Polepole alikuwa kwenye kundi la wahalifu. JPM alikosea sana kumuamini Polepole. Asinyooshee vidole wengine wakati yeye ndo mhusika mkuu.
Kuhusu ufisadi Polepole angekuwa fair kuongelea ufisadi uliofanyika kwenye awamu ya 5 ambapo yeye alikuwa mtu wa karibu na Rais. Kwanza aeleze hela za manunuzi ya viongozi wa CHADEMA zilikuwa zinatoka wapi na zilipitishwa lini na bunge? Pia aeleze zilipo trilioni kadhaa zilizoliwa kihuni na kusababisha CAG kung'olewa kihuni baada ya kuibua huo ufisadi. Aelezee pia zilikoenda pesa zilizokuwa zikilipwa kwa DPP kwa waliokuwa na kesi za uhujumu uchumi. Polepole hana usafi wala uhalali wa kuweza kusimama na kukemea ufisadi. He is a wrong messenger for the right message.