Polepole ameanza kuongea mambo ya maana ya maslahi ya nchi, sasa anaweza kutiliwa maanani

Polepole ameanza kuongea mambo ya maana ya maslahi ya nchi, sasa anaweza kutiliwa maanani

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Japo hajatubu kwa kushiriki kufinyanga demokrasia wakati wa jiwe lakini mengi anayoongea sasa yana maslahi ya taifa zaidi na sio maslahi ya chama kama ilivyokuwa mwanzo.

Kwa sasa Polepole ameanza kuitanguliza nchi mbele badala ya chama, huenda huu ukawa pia ni muelekeo wa kukitelekeza kabisa chama chake baada ya kuonyesha dalili zote dhairi kwamba hakitabadilika tena na hakina mpango huo kama ambavyo Jenerali Ulimwengu alimtahadharisha mapema kutokana na uzoefu wake mkongwe katika mojawapo ya mahojiano naye. Kwamba sasa wanamtandao wamekimeza mazima, hakitarudi tena kuwa kile chama cha jiwe.

Tuishi naye humu,
"Every saint has a past, and every sinner has a future"
 
Bado la Lissu na Ben Saanane, maana pole pole alikuwa sehemu ya viongozi wa msafara wa kifo.

Baada ya kupiga tukio la Dodoma, alipofika Dar akaanza kusifia jinsi V8 ilivyokimbia kutoka Dodoma mpaka Dar baada ya tukio la Lissu

"Unaijua vieiteee wewe... "
 
Ben Saanane wakuulizwa ni mbowe
 
Back
Top Bottom