Polepole anakosa sifa hii muhimu ndio maana hakuna anayemzingatia

Polepole anakosa sifa hii muhimu ndio maana hakuna anayemzingatia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
POLEPOLE ANAKOSA SIFA HII MUHIMU NDIO MAANA HAZINGATIWI NA WATU

Kwa Mkono wa Robert Heriel

Kwenye suala la uongozi na utawala ukitaka usizingatiwe Sana yaani upoteze mvuto licha ya watu kukusikiliza, basi kosa sifa nitakayoieleza hivi leo. Ni sifa moja kubwa Sana ambayo hiyo ndio humpa mtu ushawishi na kupata wafuasi wengi. Ukiikosa sifa hii huwezi kupata wafuasi labda ushabikiwe na Mke na watoto wako.

Polepole wengi wetu tulianza kumfahamu na bila Shaka alianza kupata nguvu ya ushawishi katika taifa letu wakati WA mchakato wa Rasimu wa Katiba Mpya. Hapo Polepole alionyesha uwezo ambao wengi walivutwa naye, Kauli zake za kujiamini zilizotoa ishara ya msimamo na kuijali jamii yake zilifanya watu waanze kumfuatilia. Pengine wengine wengi walifikiri Polepole angefaa siku moja kupewa Nafasi ya juu ndani ya taifa hili.

Hii ni kusema katika masuala ya kisiasa, utawala na uongozi ili upate wafuasi wengi na umashuhuri yakupasa uwe na MSIMAMO usioyumbishwa,

Msimamo, kutetea kile unachokiamini kiwe kizuri au kibaya ndio sifa namba moja ya kuzingatiwa ili upate wafuasi.

Wanadamu kikawaida wanahitaji mtu wa kumtumainia, kumtegemea, na ili utegemewe na kutumainiwa na wanadamu lazima uwe na sifa ya kutokuwa Kigeugeu, yaani lazima uwe na MSIMAMO.

Siku zote mtu Kigeugeu hawezi kuwa na wafuasi kwani hawamuamini, binadamu ni rahisi kumuamini adui yake ambaye anamsimamo kuliko rafiki Kigeugeu.

Rafiki Kigeugeu anasifa ya unafiki, uoga, na tabia ya kuuma na kupuliza.

Mtu mwenye msimamo siku zote haogopi matokeo ya msimamo wake. Na Hilo ndilo linalomfanya atumainiwe.
Mtu mwenye msimamo lazima awe jasiri, asiyemwoga kusimamia kile anachokiamini.
Ingawaje kila mwanadamu anakiwango chake cha lakini Mtu jasiri uoga wake uwe mdogo kabisa labda 10%.

Mifano ya watu waliopata wafuasi Kutokana na MSIMAMO usioyumbishwa uliosababishwa na ujasiri Kwa hapa Tanzania ni pamoja na Hawa;

1. Tundu Lissu.
Huyu alikuwa jasiri na mwenye msimamo mwanzo mpaka mwisho. Ndio maana mpaka Leo lipo kundi la watu linalomwamini Sana Lissu.
Ninaposema ujasiri na MSIMAMO kumbuka sijasema MSIMAMO katika nini, unaweza kuwa msimamo wa Jambo jema au Baya. Lakini msimamo ni msimamo. Ndio maana kiroho Mungu anasema uchague kuwa baridi au Moto, hataki mtu Kigeugeu (vuguvugu) Leo Moto kesho baridi.

2. Hayati Magufuli.
Huyu ni kiongozi ambaye alikuwa na msimamo mkubwa na jasiri katika hilo hakuna atakayebisha.
Mtu mwenye msimamo atakachoamua ndio hicho hicho hata Kama kitaleta matokeo mabaya.
Mtu hivi ni rahisi kupata wafuasi Kwa sababu ndivyo inavyotakiwa.

Magufuli alikuwa tayari hata kufa lakini apiganie kile alichokiamini. Hiyo ni tabia ya Kiongozi.
Ingawaje Mimi nilikuwa natofautiana na Mambo yake baadhi lakini nilikuwa rahisi kumtumainia Magufuli kuliko kutumaini mtu Kigeugeu asiye na msimamo.

Yaani ni Bora umtumaini Shetani mwenye msimamo kuliko Malaika Kigeugeu asiyeeleweka

3. Roma Mkatoliki & Nay wamitego.
Hawa ni Vijana wadogo, Wasanii lakini wanamsimamo na hawaogopi kusema kile wanachokiamini. Kupata watu wakuwatumainia ni kawaida kwani hawa huwa watetezi WA watu. Wasema ukweli.

Unajua hakuna Jambo gumu Kama kupinga na kulisema kweli mbele ya watawala.

4. jenerali Ulimwengu.
5. Mbunge Msukuma
6. Mbunge Bwege.
7. Mchungaji Anthony Lusekelo.

Miongoni mwa watu wengine wenye misimamo na kile wanachokiamini.

Ukitaka upoteze ushawishi kwenye jamii kuwa Kigeugeu.
Ukiwa unaishi Kwa kuyumbishwa hakika hakuna atakayekuzingatia.

Ukiamua kutetea mafisadi amua kutetea mafisadi, utapata wafuasi wengi tu. Na hata mafisadi wenyewe watakutumaini.
Lakini leo unatetea mafisadi kesho wenye haki unafikiri Nani atakutumaini? Hao mafisadi wenyewe watakuona huyu ni mnafiki na wenye haki nao wataona wewe ni mnafiki.

Na mnafiki Hana wafuasi.
Siku ukikutwa na shida ndio utajua kuwa mnafiki Hana wafuasi.

Shetani anawafuasi wengi, na wapo wanaomtumainia Kwa sababu anamsimamo, tangu amechagua kuwa upande wa ubaya hajawahi kusaliti kambi. Yeye ni mbaya na ndio huo ubaya, Hana unafiki.

Hata Mungu anampenda Shetani Kwa sababu ya msimamo huo.
Shetani anawafuasi wengi Kwa sababu anasifa ya muhimu ya uongozi ambayo ni MSIMAMO.

Sasa ndugu yangu POLEPOLE yeye amekosa sifa hii.
Hana MSIMAMO,
Leo anasema Katiba Mpya haina umuhimu wowote tumuache Mama afanye kazi. Kwani hicho ndicho alichokiamini kipindi kile alivyojifanya Mdau mkubwa wa Katiba Mpya?

Hata viongozi wenyewe wenye akili zilizotulia wanajua watu wenye tabia za Polepole, ukigeugeu, kutokuwa na msimamo.
Kipindi cha Magufuli, walisema Katiba Mpya sio muhimu, kaja mama wanasema vivyo hivyo, akija mwingine watasema halikadhalika.

Ndio maana Serikali makini haiwezi tishiwa na mtu Kigeugeu, serikali makini haiwezi yumbishwa na mtu anayeyumba yumba Kama Mlevi. Mara upande huu mara upande ule,

Watu wanasema mbona Serikali haimzuii Polepole kusema, hivi kuna mtu atamzuia mtu anayeyumba yumba asiseme?
Mtu asiye na Jambo analolisimamia, anayeyumba yumba ni Kama Mlevi huwezi mzuia asiseme, Leo atasema hivi kesho atakataa alichosema leo atasema alikuwa amepewa pombe.

Polepole anajifanya kuikosoa serikali(ni Haki yake na anafanya vyema) lakini anakosa kuaminiwa na kuzingatiwa na wasikilizaji wake Kwa sababu hawamuamini.
Mbona wakati wa Magufuli alikaa kimya Kama hapakuwa na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinaendelea.

Kama POLEPOLE angejipambanua Kama msema ukweli na mtu mwenye MSIMAMO tangu kipindi cha Magufuli, hivi leo watu wengi wangemuamini na kumzingatia. Lakini hakuna atakayemzingatia na serikali haiwezi kumhofia mtu asiye na MSIMAMO hata siku moja.

Atachukuliwa Kama Wale Vijana wa mitandaoni wanaoendeshwa na Hisia zao,

Ni Kama vile CHADEMA, inayumba yumba Kama Mlevi. Leo isimamie hili kesho ilikane. Doooh!!!

Acha nipumzike!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Stone town, Zanzibar
 
Ila wapo wengi TU na wenyechango mkubwa kwa taifa huja wataja🤔.
 
SIO KWELI......

Binadamu mwenye wafuasi ni binadamu anayeamua jambo sahihi lenye manufaa kwa wanaomfuata na sio mwenye msimamo tu kama unavyosema.

Yaani upate wafuasi kwa sababu una msimamo kuwa kila siku lazima unye kibarazani?


Wanaomfuata si ndio wafuasi Mkuu,
Sasa watamfuataje mtu asiye na MSIMAMO?
 
Ila wapo wengi TU na wenyechango mkubwa kwa taifa huja wataja🤔.


Ni kweli Mkuu. Ndio maana nikasema na wengineo.

Wapo watu wakiongea unajua hapa anaongea mtu ambaye atasimamia akisemacho, ambaye hawezi saliti maneno yake
 
No way, msimamo wa mtu lazima uendane na uhalisia wa wakati na usilete madhara kwa jamii anayoiongoza na yeye mwenyewe, kuwa na msimamo tu unaopingana na uhalisia hakuwezi kuwa sifa ya mtu kuaminiwa, huko ni sawa na kumuamini kichaa anaeweza kuwatumbukiza shimoni muda wowote.
 
No way, msimamo wa mtu lazima uendane na uhalisia wa wakati na usilete madhara kwa jamii anayoiongoza na yeye mwenyewe, kuwa na msimamo tu unaopingana na uhalisia hakuwezi kuwa sifa ya mtu kuaminiwa, huko ni sawa na kumuamini kichaa anaeweza kuwatumbukiza shimoni muda wowote.
Kwa kawaida msimamo unapimika, inategemea na wanaouamini na wanao utilia shaka, hapa ni umakini wa mtu dhidi ya msimamo wa mtu.
 
Hata maandiko husema unapo amua kuwamtenda dhambi tenda sana kama unazini wee ziniii wala usiwaze sio unaogopa ugopa hongera bwana mtoa mada na mi nasema hivi sitoacha kuweka picha hapa chini[emoji116]japo wadau wanasema ushamba mi sijui nitaweka mpaka nifukuzwe jf
Pic%20Layer_2021111311215721.jpg
 
SIO KWELI......

Binadamu mwenye wafuasi ni binadamu anayeamua jambo sahihi lenye manufaa kwa wanaomfuata na sio mwenye msimamo tu kama unavyosema.

Yaani upate wafuasi kwa sababu una msimamo kuwa kila siku lazima unye kibarazani?
Jini jiwe alikuwa na msimamo wa jambo baya kqbisa la kukataa scientific approach ktk kushighulikia korona. Lkn hadi leo anakumbukwa kwa ujinga wake huo
 
Back
Top Bottom