Polepole anakosa sifa hii muhimu ndio maana hakuna anayemzingatia

Msimamo ndo kila kitu.

Usimsahau Kigogo wa Twitter.

Jamaa kapoteza ushawishi mpaka huruma[emoji23]
Kwa kigogo hiyo ni case nyingine kabisa. Watu walimfuata sio kwa sababu ya msimamo bali kwa sababu ya taarifa alizokuwa ana release huku wengine mkiwa mmefyata mikia na ID zenu fake humu
 
Kiongozi ambaye siyo bora hutokana na kuangalia ujasiri wake tu !
 


Ndio maana ni Kheri umuamini kichaa au Jinni lenye MSIMAMO hata Kama ni msimamo mbaya kuliko kumuamini Mwerevu au Malaika Kigeugeu hata Kama wakati huo ametoa msimamo Mwema.

Kigeugeu Hana wafuasi.
 
Ndio maana ni Kheri umuamini kichaa au Jinni lenye MSIMAMO hata Kama ni msimamo mbaya kuliko kumuamini Mwerevu au Malaika Kigeugeu hata Kama wakati huo ametoa msimamo Mwema.

Kigeugeu Hana wafuasi.
Kumuamini mwenzako zaidi ya unavyojiamini wewe binafsi ndio mwanzo wa tatizo, huwezi kumpenda fulani kwasababu ya msimamo wake wa leo, kesho akija tofauti itabidi umgeuke, au uendelee kumuamini ila moyoni ukijua fika jamaa yako amepotea, huu kwangu ni utumwa wa fikra.
 
Jini jiwe alikuwa na msimamo wa jambo baya kqbisa la kukataa scientific approach ktk kushighulikia korona. Lkn hadi leo anakumbukwa kwa ujinga wake huo
Lazima aliyokuwa anafanya yalikuwa na manufaa kwa hao wafuasi, halafu sasa kuna mashabiki. Wao wanapenda tu kumshabikia ila si wafuasi.
 
Kuna mashabiki na wafuasi. Ni tofauti boss


Mtu anaweza akawa Mfuasi wako lakini akawa sio shabiki wako yaani hakupendi.
Ila anaimani na wewe, anakutumaini.

Na mtu anaweza akawa Mshabiki wako lakini akawa hakuamini.

Ndio maana watu wanamuamini Mungu(Wafuasi WA Mungu lakini wanaweza wasimpende yaani wasimshabikie.

Hata hivyo wapo ambao ni mashabiki na wakati huo huo ni Wafuasi.
 
True...
Ufuasi unajikita kwenye Imani na Itikadi
Ushabiki unajikita katika Upendo na mvuto.

Ingawaje wakati mwingine vinaingiliana.
 
Polepole wa wakati ule wa Bunge la Katiba na huyu wa sasa ni watu wawili tofauti kabisa! Wa sasa hana tofauti na yule msomi uchwara aliyesema Jiwe alimtoa jalalani...... AIBU, AIBU, AIBU TUPU!
 
Mbona umeitolea chadema mfano kuhusu msimamo? Vp kuhusu CCM wao wanamsimamo? Mara leo azimio la Arusha na ujamaa mara kesho azimio la Zanzibar na ubepari! Haijulikani chama kina itikadi gani!
 
Ndg hujui kumsoma mtu kwa ishara Polepole aliposema tumwache mama afanye kazi ana maana kubwa sana ambayo imejificha ndani yake
Kwahiyo kama wewe umeichukulia juu juu tu kuwa polepole anapinga katiba utakuwa umekosea sana..!
Rudia hicho kipande kutazama/kusikiliza tena.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…