Polepole angepewa ubalozi wa Mongolia, Nicaragua au El Salvado ili ajifunze kuheshimu Wakubwa

Polepole angepewa ubalozi wa Mongolia, Nicaragua au El Salvado ili ajifunze kuheshimu Wakubwa

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Natumaini kesho Polepole atasusia Kuapishwa. Sababu alisema ubunge ukiisha hagombei tena. Pia alisema ana misimamo yake haiyumbishwi wala hababaishwi na mtu yoyote.

Polepole ana bahati. Kakutana na rais Samia ana huruma. Kampeleka karibu hapo Malawi ikitaka kusalimia atapanda Basi aje Nchini.

Namshauri Rais, miezi sita ikiisha amteue mtu mwingine kuwa Balozi Malawi. Tufanye kama tulivyofanya kwa John Nchimbi. Ubalozi uyeyuke juu kwa juu kabla ya Christmas ya Mwaka huu.

Pia namshauri akishaapishwa kama atakubali, basi aende kwenye kituo chake cha kazi harakahara bil kupita kuaga aga. Kumbukumbu za kifo cha mwenda zake akawaongoze wafanyakazi wa Ubalozi huko Malawi.

Pia Polepole namuombea msamaha kwa TCRA na Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Wamruhusu na wamsamehe aendelee na Shule ya Uongozi huko malawi.

Alhaji Abdallah Majula Bulembo alishamshauli, mtu wenye hekima, upipo ukipuliza unainama. Na ule mti usioinama hung'oka na mizizi yake.

Nchimbi awamu ya pili hii inamgwaya hazitaki awepo town ila Polepole umri ule mdogo watamrusha weee akirudi mzee [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Polepole aliandaa kundi la wabunge wakiwemo akina Luhaga Mpina na Joseph Musukuma na genge lao wagomee bajeti ya serikali, mmoja baada ya mwingine wanaliwa vichwa, watafutwa wote hata kama ikibidi kuitisha uchaguzi mdogo wa ubunge.

Angepelekwa mbali kabisa halafu anyanganywe passport, mshahara apokee tarehe 70, anyimwe Hela ya umeme na maji ya nyumbani kwake, posho zote zichelewe au zisifike kabisa, asipewe wasaidizi ikiwamo dereva, awe anazurura mwenyewe, na mwisho atafutiwe vibaka wamuibie kila kitu
 
Na akitaka kwenda Malawi lazima achanjwe chanjo ya Korona taka asitake.
 
Huu ni ushauri wangu, huyu mtu akae pale miezi mitatu Kisha afukuzwe, na anyanganywe hadhi ya ubalozi.
 
Polepole aliandaa kundi la wabunge wakiwemo akina Luhaga Mpina na Joseph Musukuma na genge lao wagomee bajeti ya serikali, mmoja baada ya mwingine wanaliwa vichwa, watafutwa wote hata kama ikibidi kuitisha uchaguzi mdogo wa ubunge...
Duh sasa siwamwanbie tu arudi kijijini huko akalime
 
Polepole aliandaa kundi la wabunge wakiwemo akina Luhaga Mpina na Joseph Musukuma na genge lao wagomee bajeti ya serikali, mmoja baada ya mwingine wanaliwa vichwa, watafutwa wote hata kama ikibidi kuitisha uchaguzi mdogo wa ubunge.

Angepelekwa mbali kabisa halafu anyanganywe passport, mshahara apokee tarehe 70, anyimwe Hela ya umeme na maji ya nyumbani kwake, posho zote zichelewe au zisifike kabisa, asipewe wasaidizi ikiwamo dereva, awe anazurura mwenyewe, na mwisho atafutiwe vibaka wamuibie kila kitu
Vip unalingana nae? Au anakuzid?
 
Back
Top Bottom