Wanabodi
Nimemsikiliza HP mwanzo mwisho, hoja zake ni za ukweli na za msingi sana kuhusu kiini macho cha uchauzi wa Tanzania.
Ushauri wake watu wasijitokeze kupiga kura mpaka kwanza upatikane muafaka wa kitaifa, ni ushauri tenge kama ulivyo uwanja tenge wa uchaguzi, it's a bit too little too late! kwasababu the game is already over!,watu waliisha maliza kazi kitambo,
https://www.jamiiforums.com/threads...itaa-ccm-amekomba-almost-everything.2282068/, kilichobaki ni hiyo October 29 kwenda kuthibitisha kwa kukamilisha zile taratibu za kuhalalisha kwa kuitumia ile haki yetu ya kidemokrasia
kwa
Thamani ya Kura Yako: Je Wajua Wewe Ndiye Mwajiri wa Rais wa JMT kwa Kura Yako na Kumlipa Mshahara Wake Yeye na Serikali Yake Yote kwa Kodi Yako?.
kwa hapa tulipo,hili lori semitrela lililobeba container la uchaguzi, liko mwendo kasi kwenye mteremko, huwezi kufunga breki likasimama ghafla, ukichuna breki za ghafla, the rate of change of velocity ni direct applied to the weight of the containers and takes place to the direction ya lori linakoelekea, hivyo ukichuna breki ghafla kwenye high speed kwenye huu mteremko mkali, kwanza tairi zitawaka moto kwa friction ya lami, gari litasimama ghafla, container zitapush mbele, lori itapinduka na kila kitu kitaparaganyika!.
Madam Watanzania tumekuwa tukifanyishwa igizo la uchaguzi na NEC huku tukifanyiwa kiini macho cha ushindi wa CCM kwenye uchaguzi siku zote na chaguzi zote bila kujua kuwa ni kiini macho, ila CCM ikishinda, hata kama ni kwa kiini macho!, si hua inatuletea maendeleo ya kuonekanika?, na Watanzania tunayaona kwa macho yetu wenyewe hayo maendeleo yanayoletwa na CCM?. Sasa tunachotaka taka ni nini?, uchaguzi mkuu huru na wa haki kwenye lindi la umasikini uliotopea, au igizo la uchaguzi wa kiini macho na kutupatia maendeleo ya kuonekanika?.
Wengi humu huwa wanakuwa conscious kuhusu uchaguzi mwaka tuu wa uchaguzi kama sasa, angalieni nilishauri nini kuhusu uchaguzi wa 2020 na nilishauri lini?
Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Hapo angalieni nilisema nini kuhusu chaguzi zetu?.
Hivyo natoa wito kwa Watanzania, hiyo tarehe 29 October, twendeni tukaithibitishe tuu CCM, katika hilo igizo la mifumo, kama alivyosema Polepole!. Ile siku ile Nape alipoitoa siri hii, niliuliza kitu humu
Pre GE2025 - Kwa kauli ya Nape kuhusu chaguzi zetu, anastahili kulaumiwa au kupongezwa kwa kuusema ukweli?, sasa yanaporudiwa na Polepole, mnashangaa nini?!.
Haya mambo akina sisi, tumeyasema sana humu
- CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
- CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?
- Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla
- Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
Ni nini kipya ambacho Polepole amekisema hakijasemwa humu?.
Watanzania, uchaguzi upo, tujitokeze kwa wingi kwenda kutiki sio kutiki ili kuchagua, ni kutiki ya kuthibitisha tuu!.
Ushauri kama huu pia nilimpa Tundu Lissu
View: https://youtube.com/shorts/iv7asnge8Qo?si=GxvbLNnTPAW-OFMb
Pia nilimpa salaam Prof Kitila Mkumbo akampe Dada GE2025 - Paschal Mayala: CCM Itakuwa inapambana na kivuli chake kama CHADEMA Haitashiriki uchaguzi
Kwa sisi wa zamani enzi za chama kimoja, tumeisha shiriki uchaguzi wa rais akishindana na kivuli , hivyo tarehe 29 October, twendeni tukaithibitishe tuu kwa kutiki!.
Uchaguzi wa rais na VP tulimaliza ile January 19 pale Dodoma, matokeo ya uchaguzi wa Wabunge na madiwani, yatatangazwa leo, au kesho pale Dodoma, ukiishateuliwa na CCM, inakuwa imeisha, tarehe 29 ni kwenda tuu kuthibitisha kwa kutiki!
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali