Hii ni kutwika mtu gunia la misumari. Sisi wajumbe tumemchagua mtu kwa kura nyingi, mkatuletea wa kura 5 kisa kaunga juhudi Mkono. Mkaacha anayetekeleza ilani na kusababisha juhudi kuonekana. Wanachama wetu hawamtaki, alitutesa katika uchaguzi uliopita, hatukulala, kutwa kucha tuko kwenye kampeni kumtetea mbunge na Rais wetu, yeye anatukana na kukashifu. Leo kawa mzuri kuliko wafia chama? Wakati huohuo wwapinzani hawamtaki, kasaliti chama Chao. Leo tuambiwe tukapige kampeni la sivo hakuna uteuzi! Hizo teuzi za kutosha waliokatwa wote zitatoka wapi? Au tutaunda taifa jipya? Hiyo siyo rushwa ya teuzi? Hiki Ni chama au kambi ya jeshi, au shule na polepole ni mwalimu Mkuu?