Uchaguzi 2020 Polepole: CCM inawataka wagombea wote waliofeli kura za maoni kuwapigia kampeni washindi watakaokaidi kukosa teuzi!

Haka kajamaa kamejishushia heshima sana, sasa ndio nini icho kaongea. Mbona ni kama anajipaka kinyesi usoni. Wewe mtu kashinda kura za maoni mkamkata sababu m'memuona hafai sasa teuzi gani atakayofit mtu wa aina iyo..? Halafu kwani yeye Mungu kiasi awe na uhakika watashinda mpaka anafikia hatua ya kuwatisha wenzie tena wengine kiumri ni sawa na baba yake?? Hizo teuzi hazitolewi kwa kugawa kama maandazi.
Inatosha watuachie nchi yetu, wasituvuruge kabisa.
 
Anawataka au anawaomba......

Kwa hiyo anawafokea sio..... Ngoja wamwonyeshe muziki kwamba wao sio watu wa hovyo km yy
 
Wale watoa rushwa walikatwa?!
Vita dhidi ya rushwa ni geresha tu.

Huyo Polepole mwenyewe anachosema hapo ni ahadi ya rushwa.

Mwanachama ana wajibu wa kumpigia kampeni mgombea wa chama chake bila ahadi ya uteuzi.

Ukimletea habari keamba asipopiga kampeni hapati uteuzi na akipiga atateuliwa, unafanya uteuzi kuwa ni rushwa.
 

Duuuu kweli ccm kazi ipo. Hiyo inaonyesha utii huko ccm sio kwa ajili ya imani kwa chama na misingi yake, bali unatakiwa utii ili uzawadiwe cheo! Huwa mara nyingi nasema huko ccm hakuna nidhamu, bali kuna unafiki ili kupata cheo. Hii ndio inayosababisha ccm kufanya ukatili, ufedhuli, uhayawani na ushenzi wa wazi kwenye chaguzi zetu, ili kubaki madarakani kwa ajili vya vyeo.
 
Mwambieni Polepole wenu HASITUFOKEE.
 
Mzee naona anatangaza Teuzi kipindi hiki ambacho tunaweka kusema ni Rushwa!! yaani ukishiriki kampeni unapata UTEUZI ukigoma HUPATI.

Mambo ya kutishana!!
 
Mwambie Polepole keshaanza Serukamba kule Kigoma kahamia ACT na keshachukua fomu ya kugombea ubunge.................. pia mwambieni Membe kawaita wote waliokatwa waende ACT watapata nafasi upo wewe Polepole? akili ndogo kama kidonge cha priton
 
Ukumbuke wagombea wengi waliofeli ni watumishi wa Umma na hapo walipo July na August 2020 mishahara hawana. Kisa waliogombea uongozi wa kisiasa ndani ya CCM. Leo unakuja na gia nyingine wakawasaidie kampeni umesahau wameponea kufukuzwa kazi? Na mishahara imechukuliwa na serikali hiyo hiyo ya chama tawala?
 
Watumishi wa umma,kugombea uongozi ndani ya CCM mwaka 2020 imekuwa Kama janga la ugonjwa wa covid-19 kwao na familia zao. Kuwatambua waende Tena kusaidia kampeni ni kuwatonesha kidonda moyoni mwao.wakati wanasubiri October 28,wafanya Yao.
 
Mke anapokutukania mama halafu wazee wanakushauri umpige kwa upande wa kanga😀😀
 
Wajumbe si mulionekana mkila kuku kwa mrija? Mnanyonya supu, mko na roho ngumu,
Sisi huku tumetumia kipengele cha UZALENDO uliotukuka. Mpo.
Kapigeni kampeni
 
Mwambie polepole ajiandae tu kuwa Katibu Uenezi wa Chama Pinzani baada ya uchaguzi mkuu wa hapo October 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…