#COVID19 Polepole: Hatuwezi kuzuia watalii kwa sababu ya Corona, tutapambana nayo kama tunavyopambana na Upinzani. Nchi inategemea watalii

#COVID19 Polepole: Hatuwezi kuzuia watalii kwa sababu ya Corona, tutapambana nayo kama tunavyopambana na Upinzani. Nchi inategemea watalii

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Akihojiwa clouds Humphrey polepole amesema wapinzani Ni sawa Corona.

Kauli hii ya kiongozi kijana inaweza tafsiriwa Kama kauli ya kiongozi aliyepoteza dira na ambaye kwake maisha ya watu wasio ccm si kitu bali binadamu sahihi ni mwanaccm.

Niwaomba viongoz wa chama tawala kuchukua hatua kwake na pia vyombo vya dola kumshughulikia kwani kumwacha aendelee na tabia hii kutasababisha wapinzani nao kutumia kauli Kama hizi kujibu mapigo na hivyo kusababisha mgawanyiko kwenye taifa.

Tukumbuke ishu ya MENDE kwa wenzetu...

**********
Amesema ukizuia Watalii kuingia Nchini kwa mwezi mmoja kutokana na #coronavirus italeta shida kiuchumi, hivyo ni kuomba Mungu ugonjwa huu uondoke. #COVID19 ni sawa na wapinzani Nchini

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, amesema "Tuna vituo Nchi nzima ambavyo vimetengwa kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa ugonjwa wa virusi vya hivyo."

Kuhusu CCM kununua Wapinzani amesema "Si kweli kuwa CCM inatoa fedha kununua Wanachama wa upinzani bali inabidi wapinzani watazame jinsi wanavyoharibikiwa wenyewe ndani kwa ndani"

"Kuna mwanachama wa Mbowe anaitwa Paulina, aliondoka kwenye Chama kwasababu alikuwa anatakiwa kimahusiano na viongozi wake hivyo akaamua kuhama ili kuokoa ndoa yake lakini alivyohama wapinzani wakatafuta kisingizo kuwa amenunuliwa"

Ameongeza, "Chama cha Freeman Mbowe wanaiitana Bwana au Kamanda wao sio ndugu. Katika chama chetu huwa natumia sana neno ndugu na siyo Mheshimiwa kwa kwasababu sisi si kitu bila ya watu waliotupa dhamana"

Aidha, amesema "Hii tume ya Uchaguzi ni huru kabisa kama si huru mbona Halima Mdee na Joseph Mbilinyi walishinda? Mtu pekee anayeweza kuzungumzia kuhusu tume ya Uchaguzi ni Umma na siyo Vyama Vya Siasa."

"Tume ya utumishi wa umma ndiyo inachakata majina 5 ya Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya uchaguzi na kumpelekea Rais ili ateue jina moja"

"Freeman Mbowe anataka tufanye maridhiano lakini sisi na wao hatufikirii pamoja kwenye kile wanachohitaji wananchi hadi sasa"

"Tangu nimekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM sijawahi kufanya mkutano wa hadhara.
Sisi kama CCM huwa hatufanyi mikutano ya hadhara kwenye majimbo yasiyoongozwa na wanachama wetu, mfano Mbeya ni Jimbo la Joseph Mbilinyi yeye huwa anafanya mikutano lakini akifanya anazungumzia jela kubaya"

"Godbless Lema hajawahi kutembelea miradi ya kimaendeleo Arusha Mjini na akifanya mikutano ya hadhara hazungumzii vitu hivyo bali yeye anazungumza kuhusu Jela tu. Kila tunachokifanya wanasema ni kibaya na sisi hatukatai kushauriwa kwasababu siyo maroboti lakini tangu tumeanza kupewa ushauri hatujawahi kupewa ushauri wa maana."
 
Akigusia suala la virusi vya corona Kupitia kipindi cha SEBULENI cha Couds Plus, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema:

"Ukizuia watalii kuingia Nchini kwa mwezi mmoja italeta shida kiuchumi, kwahiyo tunaomba Mungu ugonjwa huu uondoke, Corona ni sawa na wapinzani Nchini"

"Wabunge kwa sasa wataanza kuchukuliwa vipimo kabla ya kuingia bungeni na kama wakikutwa na chembechembe za virusi vya Corona basi watachukuliwa hatua za awali kuepusha mlipuko huu"

"Tuna vituo Nchi nzima ambavyo vimetengwa kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa ugonjwa wa virusi vya Corona"

Pia soma > Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Polepole.jpg

 
It is obvious tukizuia watalii na serikali yetu ya wanyonge hatutaweza kulipa hata mishahara kwa mwezi 1. Kinachopatikana ndicho kinacholiwa.

Hela za ndani zilishaisha siku nyingi.

Ikitokea financial crisis huko ulaya na marekani huku kwetu serikali wa wanyonge itajifia yenyewe maana haitaweza kulipa mshahara kwa miezi 2.

Serikali ya wanyonge sasa inafanya ukaguzi wa kodi miaka 10 iliyopita, unashangaa unavamiwa na tra wanaomba financial records za mwaka 2010, 2009, 2011 ili tu watafte angalau kacent wanakoweza kuokoteza ili walipe tu hata mishahara.
 
Beatrice Kamugisha,
Nasema hivi bila ya kupepesa au kumung'unya maneno: POLEPOLE NI MGONJWA MWENE MTINDIO WA UBONGO, TAAHIRA NA MLEMAVU WA AKILI...!!!

Katika kipindi hichi dunia inapitia wakti mgumu kabisa cha ugonjwa wa CORONA VIRUS ukiwa umeshapoteza takribani watu elfu 8 dunia mzima ni AIBU KWA MTU AU KIONGOZI YEYOTE KUMFANANISHA MWENZAKE NA CORONA VIRUS hata Kama ni adui yake kiasi gani....!!!
Kwa hivi sasa Kuna msuguano mkali Kati ya CHINA na MAREKANI baada ya Rais Trump kusema CORONA VIRUS NI VIRUSI VYA WACHINA...!

Tunataka Mwenyekiti(T) CCM Bw. John Pombe Magufuli amfukuze kazi Bw.Polepole ya Ukatibu Mwenezi wa CCM...na asipofanya hivo Watz tutajua Magufuli ndo kamtuma aongee huo UHARO.

Meanwhile CHADEMA wajipange kwenda Mahakamani kumfungulia mashtaka Bw. Humphrey Polepole ya kudhalilisha na kukashfu CHADEMA na WATANZANIA katika mapambano dhidi ya Corona-V!

Mungu ibariki Tanzania na mlaani Polepole na CCM yake.
 
Back
Top Bottom