Anachosema kuhusu Samia wengi hawakioni hivyo. Katikati ya JPM watu walikuwa wakimshangilia JK Kila atakapojitokeza mahala. Polepole alijiona mbali sana kama JPM angekuwa hai hadi Leo. Polepole na Gwajima ndio waliokuwa wakimshauri JPM kuhusu COVID-19. Kama ingedhibika kuwa JPM alifariki kwa COVID-19 basi tungewakamata Polepole na Gwajima kwa hilo.Kwangu mimi polepole ni mjamaa na anachokitetea ni ccm isiame kwenye ujamaa moja kwa moja ingawa kiuadilifu ni kweli anachoongea natumia madhaifu yalimo kwenye ccm kwa miaka kuonyesha kuwa samia amefail...!binafsi ni kama anamuonea tu huyu mama wa watu.
Wahenga ni watu wanaotumia uzoefu wao katika kunena, kuamua na kutenda. Walisema ngoma inayovuma (toa mlio mkubwa na safi) sana ndiyo ipasukayo kwanza kisha zinafuata zile nyingine za milio ya kawaida (isiyosikika zaidi) kwa watu. Genge limemvika yeye kengele bila hata ya kuchanganya na akili zake.Imeenda hiyo!
Wahenga ni watu wanaotumia uzoefu wao katika kunena, kuamua na kutenda. Walisema ngoma inayovuma (toa mlio mkubwa na safi) sana ndiyo ipasukayo kwanza kisha zinafuata zile nyingine za milio ya kawaida (isiyosikika zaidi) kwa watu.
Lissu alipigwa risasi hapohapo, Azori alipotea hapohapo na mo dewji alitekwa hapohapo.
Hakuna hoja ya kujibu hapo kwakuwa mwenzetu ameamua kutusemea sisi watawaliwa wenzake bila kutuuliza. Ni kweli kuwa kila raia anazo haki zake analo linalomkera kuhusu watawala wake, lakini tumekubaliana kuwa wawakilishi wetu ni mabalozi wa nyumba 10/50, viongazi wa vitongoji na mitaa, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, wabunge, mawaziri, vyama vya siasa na Rais katika ngazi mbalimbali. Sisi raia kama tuna hoja zetu binafsi au kikundi tunazipeleka huko zikajadiliwe, kupimwa na kukubaliwa au kukataliwa kwa hoja ya majority. Kinyume na hapo utadhaniwa kuwa una lako jambo.Jibuni hoja zake acheni ushambenga wa kurukaruka na maneno ya kutisha na kukatisha tamaa. Mtoa post wewe ndiye unaakili Sungwi
Sasa huyo lowasa alikuwa ana jema gani?polepole mpuuzi mmoja tu, alipewa ukuu wa wilaya ya ubungo baada ya kumnanga mzee lowassa kipindi cha kampeni ya 2015. kipindi kile hakufurahi kua chini ya makonda aliekua RC wa dar es salam. hakaliziki haka kajamaa ni kanafki fulani tu.
Nawe ni zombie kumbe, wakati Magu anamteua Samia kuwa mgombea wake mwenza hicho kibichwa haikuwa na nafasi yyte CCMKinachosababisha watu wampuuze Polepole kile anachokisema kuhusu siasa ni ile historia yake ya kuwa kiongozi muhimu wakati wa serikali ya Magufuli. Polepole angeweza kumshauri Magufuli aandike katiba mpya ya serikali 3 lakini hakufanya hivyo
Polepole angeweza kumshauri Magufuli asivifungie vyama vya siasa kufanyakazi zao za kikatiba lakini hakufanya hivyo.
Polepole angeweza kumshauri Magufuli awatafute wahuni waliompiga risasi Lissu lakini hakufanya hivyo.
Polepole angeweza kumshauri Magufuli asimchague Samia kuwa makamu wa Rais wake lakini hakufanya hivyo
Polepole alikuwepo wakati mifuko ya hifadhi inaporwa fedha zake na wastaafu kukosa fedha zao lakini alikaa kimya.
Polepole anafahamu kuwa wajumbe wa Mkutano MKuu wa CCM wana akili zao timamu pengine kuliko yeye lakini yeye anawaona wajumbe wote hawana akili na hawana wanachokijua kuhusu CCM kuliko yeye.
Polepole anajikasimisha jukumu zito sana la kuitetea CCM na Tanzania bila kutaja jukumu hilo amepewa na akina nani. Yaani yeye anakijua chama kuliko wajumbe wote wa CCM na ana uchungu na tanzania kuliko watanzania wengine
Polepole alikaa kimya alipowasikia wahuni wakijitokeza hadharani kutaka kubadilisha katiba ili kuongeza muda wa ukomo wa Rais madarakani. Hoja hii haikukutana na hasira kubwa na kali kutoka kwa yeyote, kuonyesha kuwa jambo la kubadilisha katiba kuongeza muda lilikuwa linazungumzika wakati muda ukifika. Walikuwa wanapima atmosphere ya huko nje tu
Polepole huyu alikaa kimya wakati Mzee Warioba anachapwa kibao.
Polepole ni kama vile anahitaji msaada ya matibabu kuliko kumshangaa na kumsakama. Hajui kama amekalia kuti kavu kama walilokalia wezake waliowahi kukalia makuti makavu kama Mzee Makamba, Kinana, Lowasa, Mzee Aboud Jumbe, Sharif, Kingunge, Kolimba, Sumaye, Msindai, Kambona, Membe, Mrema, John Malecela, Salmin, Ali Karume, Nape na wengine wengi wasio na idadi. Anataka kuangua dafu moja kwa kuutikisa mnazi mzima. Ana umri gani yeye wa kuifahamu CCM kiasi hicho?
HahaSahihi kabisa, CCM ilimkuta na afya hii ya nywele kunyonyoka kwa ugonjwa wa juliana. Wanasemaga ugonjwa wa juliana una tabia ya kupanda kichwani.
View attachment 3440225
Polepole anaona ni heri kuchota fedha toka hazina kugharamia uchaguzi kuliko kuchangisha kwa uwazi kama vile. Anaona ni heri kuengua wagombea wa uchaguzi ili kupunguza gharama za kampeni kuliko kuchangisha kutoka watu wanaopenda amani na utulivu kwa uwekezaji wao. Hakuna mwekezaji anapenda vurugu za kisiasa zitokee nchini. Kwanini wasichangie amani yao inayolinda uwekezaji wao?Jibuni hoja zake acheni ushambenga wa kurukaruka na maneno ya kutisha na kukatisha tamaa. Mtoa post wewe ndiye unaakili Sungwi