Polepole huna sababu ya kukimbia nchi, ubalozi wa Cuba ni cheo kidogo sana

Polepole huna sababu ya kukimbia nchi, ubalozi wa Cuba ni cheo kidogo sana

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Polepole baada ya kukichafua amesema yeye hatakimbia nchi, huu unaweza kuonekana kama ujasiri mkubwa sana kwa baadhi ya watu lakini kwa wenye fikra pana hakuna ujasiri wowote kwani hakuna jambo kubwa sana ambalo limefanywa na Polepole , yeye amekubali kupoteza mshahara tu na hii imekuwa rahisi kwa sababu yeye ni mjamaa ambaye hana mafungamano sana na ukwasi mkubwa kwa hiyo haoni kama amepoteza sana. Ubalozi wa Cuba ni cheo kidogo sana kisicho na uzito mkubwa katika siasa za Tanzania, habari ya kujiuzulu kwake itakuwa imesahaulika kufikia mwisho wa mwezi ujao.

Vyeo kama vya Waziri, IGP, Jaji akijuzulu ndio itakuwa mtikisiko au kama ni balozi basi labda wa nchi kama za Marekani, Ulaya, Kenya au Uganda hivi ila sio balozi wa kituo cha Cuba. Waliokimbia nchi kama Lissu, Lema na Mbowe walikuwa ni mwiba kweli kweli kwa utawala na maisha yao yalikuwa hatarini.
 
Kama balozi ni cheo kidogo, mbona mnapanic? Mpuuzeni tu kama ana jipya.
 
Back
Top Bottom