Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Polepole
Katika kueleza jambo hili Polepole amesema "Kama watu wamefungana kura hatutarudia zoezi kwa sababu hatutafuti mshindi katika kura za maoni, tumetoa tu nafasi kwa wana CCM kuweka maoni yao ya awali ambayo yatasaidia vikao vya mbele kufanya uamuzi."
Kauli hii ya Polepole imekuja mapema baada ya kutokea kwa sintofahamu katika matokeo ya kura za maoni za baadhi ya Wagombea kufungana kwa idadi.
Mathalani, idadi ya kura za maoni za Wagombea zimegongana katika majimbo yafuatayo:
Jimbo la Mlimba
- Godwin Kunambi - 193
- Rose Rwakatare - 193
Jimbo la Mwibara
- Kangi Lugola - 173
- Charles Kajege - 173
Jimbo la Buchosa
- Dkt. Charles Tizeba - 354
- Erick Shigongo - 354