Polepole, Mangula na wengine; wakati ndio huu

Polepole, Mangula na wengine; wakati ndio huu

Halafu Chama kipya kitokane na CCM ile ile!! Kweli??? Hajui "Mtoto wa Nyoka ni Nyoka??"
Mkuu Ccm sio nyoka, Nyerere alipoweka misingi waTz tuitane ndugu, rasilimali ziwe zetu sote, ubaguzi hakuna n.k akaanzisha chama hicho hakuwa nyoka soma katiba yao, ila kimetekwa na majoka, sasa ni JUMBA BOVU,
 
Upaze sauti ya nini? Kuleta ukabila na ukanda Tanzania?

Tena tunazidi kuwatambua mmoja mmoja! Tutawarudisha wote kwenu Burundi majinga nyie
Hapa ni sheria ya historia ndio itakayoamua, hakuna nguvu itakayozuia hilo, hata ukipinga, mafisadi hamtatawala taaifa hili kwa muda mrefu sana kama mnavyoota.
 
Hicho Chama Cha Maamuzi Magumu kwa sasa ni sawa mtoto aliyekuwa kabebwa mgongoni, wakati safari ikendelea kwa kasi ya ajabu, akadhani aliye mbeba anafaidi sana.

Mtoto huyo akaamua kufanya vurugu zote ili apate kushushwa chini atembea mwenyewe mwendo wa kutoka Machi 17,2021 hadi 2O25. Tuombe, Mungu wetu, kesho atajalie viongozi wenye hekima zaidi, ukungu ukitoeka, jua litakapo chomoza tena.
 
Nawasalimu wadau wote wa jukwaa hili; ninaomba tushirikiane kwa pamoja kuangalia jambo hili kutoka pande mbalimbali na kuona kama linaweza kuwa ni uamuzi sahihi kwa majira haya ambayo taifa letu limefikia sasa...
Polepole sijui anawaonaje wanaccm wenzake.

Anawaita wahuni??
 
Upaze sauti ya nini? Kuleta ukabila na ukanda Tanzania?

Tena tunazidi kuwatambua mmoja mmoja! Tutawarudisha wote kwenu Burundi majinga nyie
Anza na Bashiru na Katibu wa ccm Mara. Na yule mwingine aliyepewa uraia kwa maagizo ya Jiwe na akateuliwa kuwa waziri
 
Binadamu bana, wakati mnakula mnafaidi kwenye ma-vieiteee mlikuwa kimya hamkutaka tusaidiane kupiga makelele mapungufu, sasa hvi mambo yamebadilika mnataka tujiunge nanyi kukemea maovu - hii siyo sahihi - sasa ni hivi kila mtu apambane na hali yake.

Sisi watanzania priority yetu kwa sasa ni katiba mpya, sasa yeyote asiyetaka katiba mpya ni adui yetu - over.
leo wanataka tuwaunge mkono😅😅😅
 
Mkuu hivi huioni chadema Kama Ni strong party to take over after the death of ccm? Mikutano inakatazwa kwa mabomu na he unahisi hicho chama kipya ndo mikutano yake itaruhusiwa na hawahawa polisi. Shida siyo chama shida Ni watu kujitoa muhanga ikitokea polisi wakakataa mikutano mnafanya hivyohivyo polisi wanawaua wote siku nyingine wanafanya wengine polisi wanaua wote, siku nyine Tena wanafanya wengine mpaka polisi watakapochoka kuua
Chadema wana ushawishi ila hawana priorities na wameonesha udhaifu kwamba wanaweza adopt uozo toka CCM hata wakipewa nchi itakuwa same old stories!

Tunataka katiba ibadilishwe kabla hatujabadili chama tawala maana bila hivyo watapoingia na wao wataweka ngumu ya kutoka huku wakitugalagaza zaidi ya CCM. Mfano halisi ni mwenyekiti wao ambaye hataki kung’atuka kwenye nafasi hio miaka nenda rudi.

I would suggest under new constitution:
-Raisi asiwe mwenyekiti wa chama kuepusha kujikita na interest za chama kuliko taifa na kuvua watu uanachama kwa kukomoa.

-Budget ya bunge isitegemee serikali.

-baraza la mawaziri litoke kwa wananchi.

-wabunge kwa wananchi.

-Tume ya uchaguzi isiwe appointed na rais.

-Watoto wa wastaafu wawe banned kushika nafasi influential za serikalini kama urais, uwaziri atleast waishie kwenye ubalozi labda na hii si kwa ubaya bali kwa manufaa ya umma. Kwa kampuni binafsi wako free kuwa hata wakurugenzi.

-Ajira za serikalini ziwe za mkataba wa 3-5 years huku maslahi yakiboreshwa ili watu wakipata uzoefu warudi kujiajiri. Mikataba iwe extended kulingana na utendaji kama mtu ana perform aongezewe muda.

-Raisi aweze kufunguliwa mashtaka na wananchi direct bila approval ya DPP.
 
Nimecheka kwa nguvu post yako namba moja, kwamba muanzishe chama kingine, lakini sio kubadili mazingira yaliyopo. Hivi mnadhani bado watanzania ni wajinga kuwa wataletewa chama kingine na ccm na bado waingie mkenge?

Nyie anzisheni chama, lakini msitegemee hawa watu wanaikubali cdm kuwa mtawateka kwa hizo porojo za uzalendo kwa uchwara, kibaya zaidi uzalendo wenu ni huo wa falsafa za Magufuli!

CCM mlishindwa kuanzisha chama mkiwa na ushawishi, mtaweza sasa wakati mnategemea wizi wa kura? Anzishenu chama hapo ndio mtajuwa watu wanajitambua.
baliana na ww, chadema ndio wameshafanya hivyo unavyosema na sasa polisi wamewafanya hivyo unavyosema Lissu hayupo nchini , Mbowe hatujui hatima yake na pengine wakatumia mwanya huo kumchelewesha kuja kujipanga na 2025, sasa niambie tunategemea nn tena na 2025 , Mungu atupe uzima, sio mbali mkuu, dawa ni kupata nguvu mpya tu,
 
Nimecheka kwa nguvu post yako namba moja, kwamba muanzishe chama kingine, lakini sio kubadili mazingira yaliyopo. Hivi mnadhani bado watanzania ni wajinga kuwa wataletewa chama kingine na ccm na bado waingie mkenge? Nyie anzisheni chama...
Uzuri wa demokrasia kuanzisha chama ni haki ya wale watakaokidhi vigezo vya kikatiba bila kuvunja sheria, sio dhambi, halafu raia watasikiliza sera za ccm, cdm na hao wapya kisha wataamua,
 
Nawasalimu wadau wote wa jukwaa hili; ninaomba tushirikiane kwa pamoja kuangalia jambo hili kutoka pande mbalimbali na kuona kama linaweza kuwa ni uamuzi sahihi kwa majira haya ambayo taifa letu limefikia sasa...
Umechambua kweli kuwa zama za ccm zimekwisha.

Lakini hao uliowataja kuwa wakombozi hawafai,ingawa umejaribu kuchanganya majambazi na wazalendo wa kweli km Nyerere na Sokoine ili kuwapa nguvu hao majambazi lakini hapa ndipo andiko lako liliposhindwa.

Magufuli na vibaraka wake km Polepole hawatatokea kuwa na mvuto wa kizalendo ata siku moja kwa maumivu waliosababisha kwa watu wasio na hatia uku uraiani.

Get it into your brain(if u have any) that Magu and his followers were marks of evils in Tanzania...it's shame to consider them as heroes!
 
Mkuu Ccm sio nyoka, Nyerere alipoweka misingi waTz tuitane ndugu, rasilimali ziwe zetu sote, ubaguzi hakuna n.k akaanzisha chama hicho hakuwa nyoka soma katiba yao, ila kimetekwa na majoka, sasa ni JUMBA BOVU,
Mkuu kumbuka watakaohama Kule CCM kuja kuanzisha Chama kipya, watakuwa wameacha makoti yao huko nyuma. Kuna siku watayakumbuka na kuyafuata.

Mimi wale wote uliowaita wazalendo wa kweli wahakikishe hivi sasa tunapata KATIBA MPYA.

Nikupe mfano: Kina Lowassa, Sumae na wengineo walitimkia Upinzani baada ya kuwa na Upinzani ndani ya CCM. Kilichowagharimu ni kwamba enzi zao walipokuwa Madarakani (ndani ya Chama Tawala) walishiriki kuvibana vyama vya Upinzani Kwa kuwatungia sheria kandamizi. Walishiriki pia kuzuia KATIBA MPYA isipatikane.

Baada ya kuona maisha ya Upinzani ni magumu waliamua kurudi nyumbani kwao CCM. Hili ni funzo tosha kwa walio na nafasi kwa sasa.
 
Kweli mkuu, ila kwa muda huu ccm lazima ifeli, muda wake ulioandikwa umetimia,
Hao nimewataja kama chanzo cha mjadala huru kuelekea mawazo mapya ya kuleta mapinduzi ya kisiasa nchini, najua ss raia tunawajua wasiofaa na wanaofaa na watakaposimama tutakubaliana kuwa huyu anafaa, hakuna litakaloshindikana tukiamua ,
 
Ni haki yenu kabisa kuanzisha chama. Ila ushindi kwa sasa haupatikani kwa sera au kwa njia ya box la kura, bali tume ya uchaguzi na vyombo vya dola ndio vinaamua nani atangazwe mshindi. Na yote haya ni mambo yanayo eleweka na wananchi. Tunasubiri hicho chama chenu tuone kikipewa upendeleo na vyombo vya dola kama ilivyo ccm. Zito alijaribu akidhani ni rahisi, kwa sasa kakabidhi chama kwa wapemba baada ya mgogoro wa CUF.
mokrasia kuanzisha chama ni haki ya wale watakaokidhi vigezo vya kikatiba bila kuvunja sheria, sio dhambi, halafu raia watasikiliza sera za ccm, cdm na hao wapya kisha wataamua,
 
Sio Bongolala land
Nchi ya watu wachovu kufikiri , chukulia mfano Samuel Sitta na Nape Nnauye wakipotaka kuanzisha chama kipya nini kilitokea
 
Back
Top Bottom