Uchaguzi 2020 Polepole na Bashiru mmechangia sana huu Uchaguzi kuwa mgumu kwa Dkt. Magufuli

Uchaguzi 2020 Polepole na Bashiru mmechangia sana huu Uchaguzi kuwa mgumu kwa Dkt. Magufuli

Hivi kweli Magufuli kwa uliyo yafanya leo wewe ni wa kuchezeshwa kisingeli jukwaani? Wewe leo ni wakupigishwa magoti jukwaani na wahuni eti mnaomba!! Mungu gani huyo mnae muomba kwa njia ya nyimbo ya singeli kama sio kumkufuru Mungu?[emoji617][emoji617][emoji617][emoji617][emoji617][emoji617][emoji617][emoji617][emoji617][emoji617][emoji617]
 
Pole pole na Bashiru walitakiwa wawepo 1990s lakini mbinu zao kwa sasa kukiwa na hii mitandao ni upuuzi
 
Bashiru, Polepole, Mpogoro hawana wanalolijua nishasema humu mara kibao! Wamemkaanga mwenzao sasa anakaangika.

Tuwe wakweli anayekipigania chama sasa hivi ni either mbunge, viti maalumu, au walioshindwa kura za maoni na waliokatwa wanaotamani kupata teuzi hapo baadae, hakuna mwananchi mmoja mmoja anayejitoa kwa ajili ya CCM kama ilivyokuwa hapo awali, ila kwakuwa hamruhusu mawazo mbadala viongozi wenu kuanzia kwenye mashina hadi mikoa hawawezi kuwaambia ukweli.

Magufuli acha ubinafsi unatuulia chama.
 
Mheshimiwa Rais Magufuli leo acha niwashitaki hawa viumbe wawili Polepole na Bashiru kwako.

Hawa ndio watu wanaofanya leo uchaguzi unakuwa mgumu kwako kutokana na mbinu yao ya ushawishi wanayoitumia kushawishi wananchi ili CCM ikubalike kwa wananchi.

Mheshimiwa Rais hebu ona walivyo kudanganya hawa viumbe wawili [emoji116][emoji116]

Wamekushawishi uzuie kampeni kwa miaka yote mitano wakijua wataua upinzani na wewe upite bila kupingwa ila unacho kiona sasa nadhani hata wewe huamini.[emoji23][emoji23]

Wamekushawishi mnunue wapinzani kwa lengo la kuugawa upinzani na kuudhoofisha ila imeshindana yaani sasa hivi upinzani wanasema kama ni chizi basi karogwa tena [emoji23][emoji23]

Wamekushawishi usionyeshe bunge laivu kwa kuwanyima wapinzani wasionekane kwa wananchi wao wakiwatetea ili wakienda majimboni kwao wananchi wawakatae ila kwa sasa hakuna mgombea anae sikilizwa kwa makini na kueleweka na wananchi wake kama mgombea wa upinzani [emoji23][emoji23]

Basi baada ya kuona hayo yote yamegonga mwamba badala watafute mbinu sahihi ila wao wameona wakushawishi utoe pesa kwa ajili ya kununua wasanii uzunguke nao jukwaani [emoji23][emoji23] wasanii hao hao unao zunguka nao jukwaani leo wakikusifia kinafiki siku akiingia Rais mwingine madarakani watamsifia na wewe kukusema hukufanya kitu.

Leo Polepole kasahau majukumu yake badala yake amekua akiwakaribisha wasanii majukwaani waje watumbuize yaani hana hoja kabisa bwana yule.

Hivi kweli Magufuli kwa uliyo yafanya leo wewe ni wa kuchezeshwa kisingeli jukwaani? Wewe leo ni wakupigishwa magoti jukwaani na wahuni eti mnaomba!! Mungu gani huyo mnae muomba kwa njia ya nyimbo ya singeli kama sio kumkufuru Mungu?

Magufuli wewe ulikuwa sio wa kubembeleza upewe miaka mingine mitano ila kwa sera za Polepole na Bashiru ndizo zilizo kufikisha hapo. Leo Bashiru ameishiwa hoja sasa hivi anazungumzia kuchukua nchi kwa njia ya dola ndio yalikuwa makubaliano yenu kwani?

Ushauri wangu kwako ukirudi madaraka hawa watu wafute kabisa na uteue wengine kwani 2025 sio mbali mambo yatakuwa magumu zaidi ya hapa.

Yote kwa yote wananchi tunafurahia sana kipindi hiki kwani hatukutegemea kama ungetoa ajira na kuahidi kulipa madeni ya wakulima na wafanyakazi. Endelea kutuneemisha baba huenda tukakufikiria fikiria kwenye sanduku la kura hiyo Octoba.
CCM kwisha kabisa kura kwa lisu
 
Back
Top Bottom