Kufuatia press conference za Polepole na yale anazungumza kwa umma kuhusu CCM na viongozi wa nchi, ni ipi itakuwa hatma ya makundi makubwa mawili ndani ya CCM?
Kwa maoni yangu, CCM ina makundi makubwa mawili yasio kubaliana ni namna gani nchi inatakiwa kuongozwa! licha ya kuwa wapo ktk chama kimoja.
Kundi la kwanza ni lile la wanazi (wanao enzi) siasa za Hayati Baba wa taifa (Jenerali ulimwengu alipata kusema wanawaita watoto wa mwalimu Nyerere), Nikimnukuu Jenerali ulimwengu watoto hao wa Mwalimu Nyerere ni Mzee Warioba, Ahmed Salim, Hayati Benjamin Mkapa, bila shaka hata Mzee Butiku atakuwa mmoja wao japo Jenerali hakumtaja. Unaweza tazama video ya mahojiano hapo chini ya Kibanda na Jenerali akifafanua dhana hii ya watoto wa Mwalimu Nyerere na mbio za urais za mwaka 1995.
Kundi la pili ni maarufu na limekuwa likisemwa sana, na kutambiulishwa kama wana mtandao, kundi hili linaonekana lili anzishwa kati mbio za urais za mwaka 1995, na linasibishwa na Rais kikwete, Hayati Lowasa, Rostam Azizi, Marehem Kingunge, Na marehemu Mzee sitta etc. Hawa walionekana kama vijana wakati wa kuzuka kwao, na bila shaka mitazamo yao kisiasa na nchi iendeshwa vipi ni tofauti na mitazamo ya Mwl Nyerere au watoto wa Nyerere, kwa maana kundi hili halikushika misingi ya kijamaa ktk siasa na uchumi kama vile kundi la kwanza wanavyoona inatakiwa kufanywa, na kwa maneno mengine kundi hili ni kama linakumbatia ubepari na democracy ya maghrib kwa kiasi kikubwa kitu ambacho ni tofauti na misingi ya CCM na ideology ya Mwl Nyerere ktk kuendesha nchi na chama.
Tujadili makundi haya watoto wa mwalimu Nyerere, kwa mujibu wa Jenerali Ulimwengu- . Bila shaka wengi katika kundi hili kama ilivyo Mwalimu Nyerere mwenyewe wana faida ya kukubalika ktk jamii kwa misingi ya uadilifu, kutolimbikiza mali, na uongozi safi...hio ndio faida ya jumla waliyo nayo mbele ya umma. Na kundi hili limekuwa likiwakosoa kundi la pili la ccm wanamtandao kwa misingi ya uadilifu, uongozi, na kujilimbikizia mali. Lakini ikitajwa misingi ya uongozi dhidi ya kundi hili kitu kimoja kisicho wazi nadhani kwa watu wengi ni kuwa watoto wa mwal Nyerere huwa wanakusudia misingi ya kijamaa, jambo ambalo binasi linanipa maswali je watanzania wangapi wako tayari kuishi katika ujamaa? Licha ya uhalali na faida waliyo kuwa nayo watoto wa Mwalimu Nyerere kwa muda mrefu, lakini nadhani kwasasa uhalali wao umepata changamoto inayotokana na jinsi awamu ya tano chini ya Hayati rais JPM ilivyo kwenda, bila shaka umma umebaki na dosari kadhaa zilizo jitokeza ktk urais wa JPM ambao umetia ukakasi wa ile faida ya uhalali wa kundi la watoto wa Nyerere kunako uadilifu na uongozi safi. Nadhani hili ndio lilossabibsuaha interview mojawapo ya Polepole kukumbana na maswali ya kuhoji uhalali wake wa kuhoji au kupinga anayo pinga sasa wakati ni mambo yalianza toka akiwa katika safu za ndani za uongozi ktk awamu ya tano. Je hili ni faida kwa CCM wana mtandao? Pili kundi hili la watoto wa Mwalimu Nyerere limekuwa likikana kupanga safu za uongozi au kugombea urais kama nime waelewa, lakini ukifuatilia mazungumzo hata ya Polepole ya hivi karibuni utagundua nao huwa wanapanga safu za uongozi au kugombea urais, mfano Polepole juzi tu amesema walimpanga Mzee Warioba kugombea urais mwaka 2015, lakini ikashindikana kwasabau alitumwa na Rais nje ya nchi akashindwa chukua fomu. Pili Ukisikiliza mahojiano hapo chini kati ya Jenerali na Kibanda, utagundua mwaka 1995 Mzee warioba, Mkapa na Jenerali walikuwa ktk mipango ya kupata urais wa nchi. Nadhani kilicho zidi tu kati yao na yale ya Kikwete na Lowasa ni kile kinachosemwa walipanga kuachiana urais, jambo ambalo halijatokea na ni wazi Kikwete alikana ahadi hio dhidi ya Lowasa.
Katika siasa za ndani ya ccm makundi haya yamekuwa yakiamuliwa/suluhu kupatikana ndani yao kwa vikao vya chama na kura za mkutano mkuu. Urais wa mama Samia ni kama umeingiza mtu pengine neutral ktk nafasi ya urais, ambae hana mizizi katika makundi haya mawili, lakini pengine kutokana na yale yaliyo jiri ktk mchakato wa kuapishwa makamu wa rais kuwa rais..huenda kundi la watoto wa Nyerere hasa team JPM wamejikuta na mgogoro na Rais na mwenyekiti wa chama...na mambo yamekwenda mpaka naona kwasasa upande wa watoto wa Nyerere kupitia Polepole ni kama wanahoji kama rais nae ni mwanamtandao au laa? Ni kama makundi haya mawili yanapambana pia kuwa karibu na Rais, haswa watoto wa mwalimu Nyerere (Rais anagombaniwa na makundi haya). Je makundi haya mawili yatapata suluhu ndani ya 2025? na vipi 2030? Na ni nini hatma ya CCM ktk mgogoro wa makundi haya? Jambo moja wanalotalkiwa pande zote mbili kukumbuka ni kuwa uimara wa nchi hii mpaka sasa upo chini ya chama chao. Hivyo ni vyema watazame picha pana ya taifa hili, hivyo wana wajibu wa kutafuta suluhu baina yao kwa maslahi ya Tanzania. Pia ni vyema siasa za fitna, uongo, uzushi zikakoma kutoka pande zote mbili.
Umma kwasasa unawatazama makundi yote mawili kwa akili za kuambiwa changaya na zako! Kwakuwa zile faida za uadilifu na kutojilimbikizia mali ktk kundi la watoto wa Mwalimu Nyerere zimepata dhoruba katika miaka 10 iliyopita, na wale umma unaweza waamini ktk kundi hili kama vile Mzee wariona tayari ni wazee kiasi cha kufikiriwa ktk uongozi wa nchi! Vijana wao waliopo mfano wa Polepole historia ina wahukumu na pengine si rahisi kupata imani waliyopata mwaka 2015 kurudi nyuma hasa ktk mchakato wa katiba mpya. Lakini ni wazi kundi hili kuna kitu linatafuta kutoka utawala wa sasa? Na wameanzisha mapambano, je CCM wana mtandao wanajipnga kujibu mapigo? Na ipi hatma ya makundi haya?
View: https://www.youtube.com/watch?v=O6Uena9vFMc