Na: Malisa GJ
Ndugu zangu waandishi, hivi mmesahau taaluma? Mbona hamuulizi “inquisitive questions” kuhusu suala la Mpina kuliwa kichwa? Ngoja niwasaidie notes kidogo. Iko hivi, Mpina ameenguliwa kwa mujibu wa kifungu cha 20(6) na (7) cha Kanuni za Maadili za mwaka 2025. Kanuni hizi zilitangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na.86 la tarehe 14/2/2025.
Tume iliita vyama vya siasa kusaini kanuni hizo. Chadema tulikataa kusaini kwa sababu zilikuwa na mapungufu mengi. Na tukashauri vyama vingine vigome kusaini pia, mpaka pale kanuni hizo zitakapofanyiwa marekebisho kwanza (Na hiyo ndio maana ya No Reforms No Election). Lakini wazee wa “project” wakaenda kusaini kwa mbwembwe. Kusaini means walikubaliana na yote yaliyopo.
Sasa kanuni zilezile walizosaini ndiyo zimetumika kuwala vichwa. Sasa waandishi, kwa nini hamuulizi hili swali? Muulizeni Ado analia nini wakati alisaini kanuni mwenyewe? Chadema tuliposema kanuni zina mapungufu walitutukana na kusema tumekimbia uchaguzi. Leo yamewakuta, wanarudi kwa wananchi kulia. Ndiyo maana Boniyai amesema hawa watu wanapenda michezo ya . Bata, Wahed.!