Litakuwa jambo jema sana, ila kinachonishangaza katia serikali hii, viongozi wa chama wamekuwa ndo wasemaji wa serikali.
Kuna miradi mingi sana inayotekelezwa na serikali kwa kodi za wananchi, na hiyo miradi inatekelezwa maeneo ambayo kuna watumishi wa serikali waliopewa mamlaka na serikali kusimamia na kuwa wasemeji katika maeneo hayo, cha ajabu ni kwamba hawa watendaji wa chama wamekuwa ndo wasemaji wakuukatika mambo mengi na kuwaacha wahusika pembeni.
Wamekuwa ndo wanaokuja kukagua miradi wakati kuna watu walioajiriwa na serikali kufanya hizo kazi, Mbaya zaidi, kutokana na kutokuwa na taaluma na ufahamu katika fani mbalimbali, wamekuwa wakiwahukumu/kutoa taarifa ambazo kitaalamu si sahihi kwa mkuu wao na watu wengi wamakuwa wakiadhibiwa bila makosa, Kisa ni kampeni.