Polepole pole ila Omba japo Msamaha Ulitukwaza wengi

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mheshimiwa Polepole kilio chake cha kuzimwa kwa sauti yake kinakisikika ila kwa hakika tunashindwa kumuelewa.



Kwa hakika kilio kama chake leo, kimekuwa chetu muda wote hata kipindi yeye akiwa mshirika mkuu wa mamlaka katika kutunyamazisha.

Ikumbukwe Mh. Polepole alikuwa huyu hapa katika ubora wake:

Your browser is not able to display this video.


Alisahau kuwa na sisi tulikuwa na haki za kupaza sauti zetu kwa mujibu wa katiba hata kama binafsi hakuzipenda.

Hatupendi anavyonyamazishwa mheshimiwa huyu ila sasa angalau tusikie neno lake la kujutia basi?

Your browser is not able to display this video.


Angalau tuone basi kuwa sasa anatambua alitukosoea mno kama hatimaye naye leo amepata kugundua kuwa wanamkukosea haki.

Ni hayo tu kwake mheshimiwa Polepole.

Atafakari achukue hatua.
 
Huyu muheshimiwa sijui kama kuna mtu atakuja kumpita kwa uongo ambao ameshawadanganya watanganyika
 
Ataomba msamaha 2026 baada ya kupokea pensheni yake ya ubunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…