Mimi ningekuwa niko kwenye jopo la washauri wa Samia ningemshauri kwamba kuna haja ya yeye kuli address taifa kwa masaa yasiopungua mawili kufuatia hali inayoendelea hapa nchini kwa sasa.
Matukio ya kuogofya yanazidi kuongezeka kila kukicha na yanahusishwa moja kwa moja na serikali..
Chuki dhidi ya serikali inazidi kuongezeka tu kila iitwapo leo, sasa hivi imefika stage yaan mtu ukiongea kwa kuisifia tu hii serikali raia wanatamani wakupige makofi kma sio kukutenga.
Serikali imepoteza ushawishi mkubwa kwa raia na hasa wanainchi wa hali ya chini yaani wanyonge, wengi wao wanaona wametengwa na serikali yao.
Licha ya raisi kuonesha jitihada za kusaidia wanainchi kwenye masuala muhimu kma ajira, ila bado jitihada hizo matunda yake hayajawafikia watu wengi hasa vijana.
Kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi kwa watumishi wake wa ngazi za juu wakati huo mahosipitalini hakuna dawa wala vifaa tiba toshelezi, vijana hawana ajira wala mitaji ya kujiajiri.
Vijana wengi wana hasira sana na serikali yao na sasa hivi wameshafikia kwenye point ya nihilism yaan wanaona maisha hayana maana tena wameshakata tamaa, na sababu kuu ya wao kukata tamaa hivi ni kupuuzwa na serikali yao, na wakishafikia hatua hii lazima wajaribu kufanya mageuzi ya serikali hata kama itagharimu maisha yao.
Hivyo basi kwa sababu hizo hapo juu Ningemshauri Samia aachane kabisa na kiburi cha dola kwamba eti yeye ndio amri jeshi mkuu...
Inapaswa akae atafakari sana afanyie kazi chanzo cha huu upepo mbaya unaovuma kwa kwa sasa ambao unaweza kumfanya akawa ni raisi mwenye historia mbaya zaidi kwenye taifa hili, kitu ambacho kitawafanya watanzania wakose imani na raisi mwanamke huko mbeleni.