Polepole: Unafiki ni sehemu ya maisha kwenye siasa hauepukiki awataka wanachama kutii kanuni hata kama ni kinafiki

Polepole: Unafiki ni sehemu ya maisha kwenye siasa hauepukiki awataka wanachama kutii kanuni hata kama ni kinafiki

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwenezi Polepole ambaye pia ni mlezi wa chama mkoa wa Arusha amewataka wabunge kuendelea kukutana na wananchi na kukamilisha ahadi walizotoa mwaka 2015.
Hata hivyo Polepole amezuia watu wengine kufanya mkutano na wananchi kana kwamba wao ni wabunge.

Polepole amewaruhusu wabunge kuwanunulia wananchi maji wakati wa mkutano kwa sababu utaratibu huo umekuwa ukitumika wakati wote.

Wakati huo huo Polepole amewataka wanachama wake kutii kanuni na maagizo hata kama watafanya hivyo kinafiki.
Unafiki ni sehemu ya tabia ya binadamu katika maisha hivyo kama inakuwia vigumu kutii kanuni na maagizo basi jaribu kutii hata kwa kinafiki tu mambo yataenda, amemalizia ndugu Polepole.

Source Channel ten tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom