GE2025 Polepole unapomshauri Samia aseme nini kwenye kampeni, unatuona sisi Watanzania ni mazuzu?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kama wanachama wa CHADEMA iliyoanzishwa 1992 wanaitwa "nyumbu" kwa kutapeliwa na
Polepole, je Watanzania tunaoendelea kutapeliwa na TANU/CCM tangu 1961 tunaitwa nani!!??
Kwa hiyo wanaCCM wakitapeliwa inatoa uhalali wa wanaCHADEMA kutapeliwa? Mkiitwa CCM B mnachukia.
 
Upumbavu ni kuamini polepole anawapambania wananchi
 
Upumbavu ni kuamini polepole anawapambania wananchi

Upumbavu ni kudhani mtu anaweza kumsemea mwingine. Bila kusahau anachokisema mtu sasa, si jana; hicho ndicho kinachohesabika!



Kwani huyu ndugu anasema je leo vile?
 
Najaribu kupata point Yako lakini nashindwa.
 
Duh
 
Bahati mbaya siasa za nchi yetu zina watu wengi sana bendera fata upepo hawajui lolote zaidi yakufata fulani kasema nini.

Hii nchi ukipendwa hata kama unaongea pumba utasifiwa wala hawataangaika na kile unachosema zaidi ya kuangalia nani kasema.

Polepole alijua akimsifia Lissu atapata wafuasi wengi sana mtandaoni hata kama zingine akiongea ni pumba bado atapigiwa makofi.

Ila kwa wenye akili hawawezi kupoteza muda kumsikiliza polepole au kumakinika nae.Lazima wangeendelea na harakati zao wanazoona zitazaa matunda.
 

Machawa wamefungiwa walivyo block jamii angalia unaongea na nani! Hakuna ushabiki sasa ni hoja tu
 
Shida ya CHADEMA. Baadhi yenu mna akili ndogo na kutokana na akili ndogo mtachukua muda sana kupata madaraka ktk nchi hii

Mnamuamini kila mtu ilimradi tu kaonesha dalili za kuipinga ccm leo hii ata mwigulu nchemba akianza kumponda mama mtamshabikia na kusahau yote na huu ndo ujinga wenu
Mnamuamini mtu yyte yule kisa kaongea maneno mnayotaka kusikia
 
Wewe kila comment yako ni
Polepole kwa sasa ni shujaa wa nyumbu za CHADEMA. Nyumbu zilimtukana LEMA kisa kampinga Polepole. Hakuna watu warahisi kupotezwa mwelekeo kama wanachama wa CHADEMA. Ni watu waliozoea kutapeliwa.
Wewe kila comment yako ni Chadema, walikufanya hilo lisilopona?
 
Reactions: Lax
binafsi toka mwanzo nikikua napinga vikali polepole kupewa title ya "shujaa".

Hata hiyo kumuongelea Lissu ilimchukua muda --- nadhani alipiga tathmini kwamba kwa hali ilivyo support inahitajika

Mimi kadili navyoona polepole anamashabiki wengi ndo nazidi kuamini. ccm bado ipo sana , na mabadiliko yatachukua muda.

toka aanze hii harakati nimeskiliza sana, ni mjanja mjanja tu
 
When a charlan fights a charlatan, the result is a comedy of errors.
 
Yule anarukaruka tu hasemi yenye hatari.

Ameshapima akili za wanaomuunga mkono wanapenda kusikia nini basi ndio anawalisha iko iko.

Kuna wale waandishi wa habari wawili Zungu na yule wa Star tv waliwahi kumuweka kwenye kibano hadi alitoa mlio.

Mtu aliekuwa anaihubiri haki akapata nafasi akakaa kimya baada yakuona kawekwa mbali na keki aliyokuwa nayo anarudi kwenye uanaharakati.Mtu wa namna hii siwezi kumuamini kabsa.

Yeye atulie aache wanaopambana na CCM wakiwa ndani hapa waendelee kupambana.

Kwangu Melo ni shujaa sana maana anapitia mengi lakini wala hakati tamaa wala hajabadilika.

Melo akiamua kuuza taarifa za watu humu basi naamini anakuwa tajiri mkubwa fasta tu.
 
Reactions: Lax
Upumbavu ni kuamini polepole anawapambania wananchi
Mnataka mpiganiwe kivipi? Ameeleza dhulma ya CCM ambayo kila mtu anajua na amekiri. Tatizo la watanzania wengi hasa watanganyika wanaongea kwa sababu wana midomo tu. Polepole ameongea yale ambayo siku zote tunayalalamikia, bado watu hawaamini, kwani hao akina Wasira ambaye ni makamu mwenyekiti hawakuwahi kusema CCM inaiba kura? Ulitaka tusiamini? Ndiyo wote wana shida zao lakini hii haitukatazi kumwamini Polepole hata kama alilosema ni dogo.....Linatosha. Suala la kupambana......tutapambana sisi wenyewe, hatutaki mtu mmoja wa kutupambania. Umeshahongwa tayari.
 
Reactions: Lax
Tatizo la HP yeye anataka watoke asiowapenda abaki na kundi lake waendelee wao..!!
 
Reactions: Lax
Mpaka sasa kaongea nini la maana polepole?

Mimi ni mdau wa mabadiliko pia , nachokushauri msikilize kwa makini sana 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…