Polepole: Vyombo vya ulinzi na usalama tunzeni kila taarifa ya matumizi mabaya ya madaraka ya mtu yoyote. Hatutaka kusikia zimepotea

Polepole: Vyombo vya ulinzi na usalama tunzeni kila taarifa ya matumizi mabaya ya madaraka ya mtu yoyote. Hatutaka kusikia zimepotea

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Vyombo vya ulinzi na usalama kwa maana ya usalama wa taifa, jeshi la wanannchi, jeshi la polisi, takukuru, jeshi la uhamiaji tuzeni kila kipisi, bunje ya taarifa ya matumizi mabaya ya madaraka ya mtu yoyote iko siku inakuja tutataka hesabu kwa kila mtu aliyekuwepo kwenye vyombo na mwenye dhamana ya kutunza taarifa hizi.

Hatutaka kusikia zimepotea, azionekani na zitapotea na wewe kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi yetu,
Polepole


 
Nasikia kile kikosi cha wavaa mizura amesema kinaongozwa kijana wake?
 
Yule Mzimbabwe alifikaje Ikulu mtu mwenye kasha ya rushwampaka puani?
Screenshot_2025-09-03-21-59-30-42_0b2fce7a16bf2b728d6ffa28c8d60efb.jpg
Screenshot_2025-09-03-21-57-57-91_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Safi sana Polepole, endelea kuwakalia wahuni shingoni hivo hivo.
 
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ameshauri vyombo vya ulinzi na usalama vikiwemo Jeshi la Wananchi, Idara ya Usalama, Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na Uhamiaji, kutunza kila taarifa na hata punje ya karatasi inayohusisha matumizi mabaya ya madaraka.
 
Binafsi naungana na Balozi aliyefukuzwa kutoa ushauri huu. Siku hazigandi. Ipo Siku inakuja waliotumia madaraka kujinufaisha watafika mbele ya mkono wa sheria na watawajibika kwa matendo Yao.

Kila la heri mnaondelea kula keki ya taifa kwa sasa.
 
Samia anajua ili ndio maana kashajiandalia dubai na omani na siku mnakuja kumshika mnaambiwa sio raia wa tz
 
Screenshot_20250909-091807_Google.jpg


Mzee wa Kubanaga huwa anasisitiza sana kwa mtu mwenye mamlaka au nafasi fulani katika kazi yake basi ahakikishe anatunza taarifa zake vizuri. Iwe ni kipisi cha karatasi au kipande cha taarifa ahakikishe anakihifadhi kwani ipo siku isiyo na jina kila mtu atakuja kuulizwa.

Kwa namna anavyosema ni kana kwamba anamjua mtu ambaye siku moja atakuja kushika madaraka ya nchi na atawashitaki na kuwawajibisha wahusika wote.

Inasemwa pia kama kuna madudu ya huko nyuma katika awamu iliyopita basi nae atakuwepo kwa sababu alikuwa sehemu ya mfuko au msaidizi wa mkuu wa kaya,kama ambavyo mwenyewe amejieleza mara nyingi

Je swali la msingi,ipo siku Tanzania itakuja kuwa na kiongozi ambaye atajivika ngozi ya Chui na kuwararua wote waliofanya ufisadi?

Je, ipo siku Tanzania itakuwa na kiongozi ambaye atafilisi mali zote zilizo patikana kwa ufisadi?

Muda utaongea

Ni hayo tu!
 
Unajua mifano hipo kwa watu wachini lakini huu mfano wa Neno umepotea sio kwa mtu wa chini hata serikali imepotea
 
View attachment 3468135

Mzee wa Kubanaga huwa anasisitiza sana kwa mtu mwenye mamlaka au nafasi fulani katika kazi yake basi ahakikishe anatunza taarifa zake vizuri. Iwe ni kipisi cha karatasi au kipande cha taarifa ahakikishe anakihifadhi kwani ipo siku isiyo na jina kila mtu atakuja kuulizwa.

Kwa namna anavyosema ni kana kwamba anamjua mtu ambaye siku moja atakuja kushika madaraka ya nchi na atawashitaki na kuwawajibisha wahusika wote.

Inasemwa pia kama kuna madudu ya huko nyuma katika awamu iliyopita basi nae atakuwepo kwa sababu alikuwa sehemu ya mfuko au msaidizi wa mkuu wa kaya,kama ambavyo mwenyewe amejieleza mara nyingi

Je swali la msingi,ipo siku Tanzania itakuja kuwa na kiongozi ambaye atajivika ngozi ya Chui na kuwararua wote waliofanya ufisadi?

Je, ipo siku Tanzania itakuwa na kiongozi ambaye atafilisi mali zote zilizo patikana kwa ufisadi?

Muda utaongea

Ni hayo tu!
Anachimba biti
 
Back
Top Bottom