Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Yule Mzimbabwe alifikaje Ikulu mtu mwenye kasha ya rushwampaka puani?
Anachimba bitiView attachment 3468135
Mzee wa Kubanaga huwa anasisitiza sana kwa mtu mwenye mamlaka au nafasi fulani katika kazi yake basi ahakikishe anatunza taarifa zake vizuri. Iwe ni kipisi cha karatasi au kipande cha taarifa ahakikishe anakihifadhi kwani ipo siku isiyo na jina kila mtu atakuja kuulizwa.
Kwa namna anavyosema ni kana kwamba anamjua mtu ambaye siku moja atakuja kushika madaraka ya nchi na atawashitaki na kuwawajibisha wahusika wote.
Inasemwa pia kama kuna madudu ya huko nyuma katika awamu iliyopita basi nae atakuwepo kwa sababu alikuwa sehemu ya mfuko au msaidizi wa mkuu wa kaya,kama ambavyo mwenyewe amejieleza mara nyingi
Je swali la msingi,ipo siku Tanzania itakuja kuwa na kiongozi ambaye atajivika ngozi ya Chui na kuwararua wote waliofanya ufisadi?
Je, ipo siku Tanzania itakuwa na kiongozi ambaye atafilisi mali zote zilizo patikana kwa ufisadi?
Muda utaongea
Ni hayo tu!