Polestar 5 EV Sedan imezinduliwa: Mswiden na Mchina wanatuuzia kwa Mil 320 bila TRA!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Bado tupo IAA Mobility Ujerumani, na sasa tunaona kampuni ya magari Polestar kutoka Sweden, wakizindua flagship sedan yao Polestar 5.

Polestar 5 GT zimezinduliwa za trims mbili, Dual Motors Launch Edition na Performance Launch Edition.

Acceleration kutoka 0-100 kph inachukua sek 3.8 tu kwa Dual motor na 3.1 tu kwa Performance model, ila zote zinaishia 250 km/h. Na power, Dual Motors ina 748 hp na Performance ina 884 hp.

Polestar 5 ina battery la 112kWh linalosafiri hadi 670 km kwa Dual motor Edition na 565 km kwa Performance Edition. Na pia, imeundwa kwa 800V architecture kwahiyo kuchaji 10-80% inachukua dk 22 tu (charging speed ya 350kW)!

Kwa ndani, kuna 14 inch screen touchscreen ikiwa na Android Automotive OS with Google built-in, na kuna 9 inch screen kwaajili ya dereva, na HUD.

Kwa wapenzi wa music, utachagua speaker 10 au 21 kutoka Bowers & Wilkins.

Driver assistance systems ipo ya Pilot Assist ambayo ina adaptive lane positioning ukiwa kwenye speed hadi ya 150 km/h. Pia kuna radars, camera na sensors, airbags nane, na driver monitoring system.

Mwisho kuhusu bei, Dual Motor Edition itauzwa Tsh 250 na Performance Edition itauzwa Tsh 320 Mil.
 
aya mambo ntaishia kuyasoma tu na kuangalia mapicha picha daaah so sad.......!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…