Wadau, Polisi wetu ni Wahuni, Yes, they are Hooligans! MAra nyingine huwa nafikiri kuwa hawa jamaa huwa wanakusanywa tu vijiweni na kupelekwa CCP na baadaye kupewa ajira!
Kwa waliooona taarifa ya habari wiki ilopita wakati CDM Arusha walipoandamana kwenye mazishi kuna clip moja inaonyesha tukio la tarehe 5 Januari, Asikari Polisi wakilishambulia gari VV nyekundu ya Mfuasi wa CDM! Yaani wanalipiga gari kwenmye vioo na magongo yao!
Ajabu ni kuwa hata maandamano ya mazishi yale, Polisi waliyapiga marufuku lakini kwa kuwa walishaonja nguvu ya umma tarhe 5 Januari ilibidi wavumilie hata pale CDM walipoandamana kutoka Motuary hadi NMC. Ajabu ni kuwa yalikuwa maandamano ya amani sana tena bila Polisi. Polisi wetu huwu wanapima maji ili kutesti nguvu ya umma na bila shaka wameshagundua kuwa Umma kwa sasa hauogopi tena.
Huwa nawasikitikia sana Polisi wetu ni kama vile huwa wanatakiwa wavute bangi kabla ya kwenda kwenye 'kutuliza fujo;.