Police to investigate persons named in UN's Experts Report!

Binafsi sioni haja kupoteza rasilimali ikiwemo muda na mategemeo ya watu kumchunguza mtuhumiwa ambaye hata kipofu angemtambua kutokana na historia ya uhalifu wake usioacha nyayo hata chembe. Hii ni kanyaboya. Ukisoma taarifa ya wataalamu kwa umakini, ukatumia kumbukumbu nzuri na si akili, maarifa wala nyenzo; utamwona vizuri tu huyo mtuhumiwa
 


Safi ndugu yangu Du!! huyu jamaa itakuwa kama EPA kesi haishi mpaka Mzee walalahoi wataipinga kwa nguvu zao mpaka waende kaburini kesi itakuwa pale pale .
 
Mwema unaweza kuchunguza mawaziri wengine wakiwa wakuu wa wizara iliyo juu yako?? Unaweza kuchunguza idara ya usalama especially viongozi wake wakuu???
Unaweza kuchunguza king makers wa TZ??

Acha kutusumbua na kudhani wote ni mabwege hapa
 
Mwema unaweza kuchunguza mawaziri wengine wakiwa wakuu wa wizara iliyo juu yako?? Unaweza kuchunguza idara ya usalama especially viongozi wake wakuu???
Unaweza kuchunguza king makers wa TZ??

Acha kutusumbua na kudhani wote ni mabwege hapa

Kama wa EPA hawakamatiki, basi tutarajie kuwa huko tuendako tutapata stori kama za EPA, kuwa walanguzi wa Silaha pia hawakamatiki. Tutahatarisha usalama wa Taifa. Ya nini kujisumbua Mwema si ungekaa kimya tu?, hii style ya kujisafisha imeprove failure from mwanzo
 
Kwa kifupi nchi haina viongozi wenye busara. Balaa kubwa hili Tanzania. Kila mmoja anaongea lake lisiloeleweka wala kuaminika. Ushindwe kuwachunguza waliochukua fedha BOT wakafanyia biashara laini na kuhonga vibinti magari utokee na uajsiri wa kumchunguza na kumtia ndani aliyezitumia kununua kifaru?? Upuuzi huu hauna tofauti na jogoo awikae saa saba usiku!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…