Polisi amefariki kwa kupigwa manati

Polisi amefariki kwa kupigwa manati

Siumeona kipago wameshika watu 3[emoji23][emoji1787] huko wanaovuta jiwe sijui ni wangapi

Watumiaji lazima wavae gloves, helmet na wafuzu mafunzo Cuba au zamani wangeenda Yugoslavia
 
Ila Kenya ndugu zetu wana mambo mazito kweli kweli. Kuna askari kapigwa manati katika maandamano akafariki.

Hebu angalia hiyo manati kwenye picha[emoji1787][emoji23], Mungu anisamehe.

===

View attachment 2573055
Afisa wa Polisi amefariki baada ya kupigwa na jiwe kifuani wakati wa maandamano ya kupinga Serikali Alhamisi, katika Kaunti ya Kisumu nchini Kenya.

Ben Oduor, ambaye alikuwa amelazwa katika Kituo cha Polisi cha Keroka katika Kaunti ya Nyamira, alifariki katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi cha Hospitali ya Aga Khan (ICU) Alhamisi usiku.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Nyanza Noah Mwivanda, alisema Koplo huyo aligongwa na watu waliotumia manati kubwa ya kujitengenezea ya kienyeji na mawe walipokuwa wakiendesha mapambano na Polisi.
Manati ni silaha mojawapo hatari sana kati ya nyingi hasa zikitumika gololi. Kichwani huponi
 
Tatizo la Kenya ni ubaguzi wa kikabila, pengine huyo Pot angepona. Hilo jina BEN ODOUR linafanana na watu wa kabila la Odinga, sasa usikute Jeshi na Serikali vilimsusa Afande Oduor ajifie kwasababu nduguze ndo wanasumbua nchi. Nimefanya kufikiria tu. 🤔
 
Kwa Manati hiyo siyo Polisi tu hata Mwanajeshi lazima aende Kuzimu
 
Back
Top Bottom