Polisi anayepokea rushwa tabia hiyo ametoka nayo kwenye malezi

Polisi anayepokea rushwa tabia hiyo ametoka nayo kwenye malezi

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
''Askari ambaye anapokea rushwa hiyo tabia ametoka nayo kwenye malezi na wananchi ndio wamekuwa wakichochea polisi kuchukua rushwa'' - Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David Misime

Je kweri wananchi ndo wanachochea polisi kuchukua rushwa.
 
Rushwa ni ya mfumo. Kama kosa la traffic ni 30,000 na nikimpa 10,000 ananiachia, what do you expect of a human being with no piece of washing soap at home? Nimserve 20 na bado tajiri mwenye gari anahitaji 40,00 per day. Utafanyaje?

Pendekeza katika scenario kama hiyo tufanyeje kuzuia kuta rushwa
 
Sio "kweri" bali ni "kweli".

Ndio ni kweli wananchi ndio wanachochea hizo tabia na sio kwa polisi tu bali karibia kwenye kila idara. Kuna matendo watu wengi tunafanya kwa kuhisi ni utamaduni kumbe ni rushwa mfano kutoa ela (kifuta jasho) baada ya kupewa huduma na mtumishi wa umma (polisi, daktari nk) kwa kuhisi ni msaada kakufanyia wakati ni wajibu wake.
Pia wananchi tumeisha jijengea mitazamo ya kwamba ukiwa asikari (hasa trafiki) wewe umehula na ili mambo yako yaende haraka haraka na yafanikiwe (iwe ni kesi kituo cha polisi au barabarani) lazma utoe kitu kidogo ili kumhamasisha polisi husika kusimamia mambo yako.

Kwani umesahau kuna kiongozi aliwai sema tuwe tunawapa marafiki ela ya kufutia vumbia? Hii ni rushwa pia ambayo tumeitamadunisha
 
Rushwa ni ya mfumo. Kama kosa la traffic ni 30,000 na nikimpa 10,000 ananiachia, what do you expect of a human being with no piece of washing soap at home? Nimserve 20 na bado tajiri mwenye gari anahitaji 40,00 per day. Utafanyaje?

Pendekeza katika scenario kama hiyo tufanyeje kuzuia kuta rushwa
Upigwe fine bila kosa?
 
Back
Top Bottom