Wana JF kama mnakumbuka juzi niliandika uzi unao elezea tukio la polis kumuua raia kwa kumpga risasi maeneo ya Sokon one Arusha,jana polisi wamejibu kwa humu JF kwa kutumia jina la mandieta,sasa mimi nataka kuwaeleza ukweli wa mambo maana mimi nakaa jirani na eneo la tukio hilo na nilikuepo na nilishuhudia polisi wakifyatua risasi.
Ilikua ni majira ya kama saa 3 asubuhi marehemu alikua amekaa nje ya nyumba anayoishi alikua anachezea simu yake ya mkononi ndipo wakatokea watu 3 walio vaa nguo za kiraia wawili walikua na bunduki na walipo mfikia marehem karibu waka mwambia leo ndio arubaini yako mwenzio tulisha muua kwa risasi na wewe nilazima ufe,marehem akasimama na kuwauliza kwani vipi wazee? ndipo hapo polisi wakamfyatulia risasi na nyingine wakaendelea kuzipga juu ili raia wasisogee eneo lile.Baada ya hapo nikaona polisi mmoja akimpekua marehem kwenye mifuko ya suruali yake na kutoa wallet na kitambaa na baadae ilikuja gari ya polisi na kuuchukua mwili wa marehem bila na kuingia ndani kupekua bila search warrant wala balozi hakuwepo.