beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,377
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz ameelezea kuhusu hali ya usalama nchini kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi Septemba 2019 ikilinganishwa na mwaka 2011 hadi 2015.
Amesema “Makosa makubwa ya Jinai yameshuka kwa asilimia 24.7. Makosa makubwa kwa mfano mauaji yameshuka kwa asilimia 26. Kwa miaka minne ya kwanza makosa ya mauaji yalikuwa 14,960 lakini katika miaka minne ya mwisho yaani katika utawala huu, mauaji ni 10,972”
Aidha, amebainisha “Makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha (armed robbery) yameshuka kwa asilimia 54.2 hiyo ni zaidi ya nusu. Miaka minne kabla ya utawala huu makosa ya kutumia silaha yalikuwa 4,515 lakini katika kipindi hiki cha miaka minne makosa hayo yameshuka kwa 2,070”
Ameongeza “Makosa ya usalama barabara nayo yameshuka kwa kiasi kukubwa, katika kipindi cha miaka kuanzia 2011 hadi 2015 yalikuwa 73,871 na ukilinganisha na makosa 22,621 kati ya 2015 hadi Septemba mwaka huu ambayo ni sawa na upungufu wa asilimia 69.4”
Amemalizia kwa kusema “Ndio maana nasema kwa ujumla hali ya nchi yetu ni ya amani na utulivu”