Mabibi na mabwana niko safarini kuelekea pande za Burigi katika kutia shime juhudi za kizalendo zenye mashiko zilizoasisiwa na hayati mzee baba katika kulisukuma gurudumu la utalii wa ndani, mbele.
Niliyoyashudia njiani hasa kuwahusu wale waliozowea kubrashi viatu kwa kutumia pesa za wengine, dhidi ya wale wasiokuwa na ubavu wa kujisimamia wenyewe, yananisukuma kuuleta uzi huu.
Ili kupata takwimu za kutosha kuhusiana na uzi huu kwa maana ya methodology wahanga wote waliachwa kupambana na hali zao (hapana kuingilia), pia uchukuaji picha ulikuwa ni wa kuepukwa kuchelea vipigo vya mbwa koko.
Hiiiiii bagosha. Dhuluma tupu. Mama Samia ana kazi nzito. Yanayotokea si bure!
Kesi mkononi ni 'Nyakanazi' juzi kwenye: "operation rasmi inayosemekana kuendelea ya kukusanya 30,000/= kwa kila gari. Magari lengwa zaidi ni ma Fuso, Mabasi (makubwa kwa madogo) vi probox, Noah, nk na kina yakhe wengine wanaoweza wakajingiza wenyewe kwenye anga zao. Mamwela wameweka foleni ya magari yenye urefu upatao mita 100. Kikosi kazi kimejizatiti - "Kazi inaendelea!"
Binafsi nikisubiria kuhudumiwa kama wanavyodai wenyewe niliyashudia haya:
1. Magari ya abiria kutozwa faini ati kuwa palikuwa na baadhi ya abiria (hata mmoja tu bila kujali alikaa wapi) kuwa hawakufunga mikanda.
2. Magari ya abiria kutozwa faini ati kuwa kuna mafurushi hata ya nguo za wale wanyonge wa mwendazake wasiokuwa na uwezo wa kumudu mabegi na masanduku mazuri mazuri ya kukokota yaliyo maarufu sana kwenye viwanja vya madege.
3. Magari kutozwa faini kwa sababu ya kuwepo crack yenye size yoyote kwenye taa au kioo chochote.
4. Magari kutozwa faini kwa kutokuwa na mikanda au kutokuwa na mkanda mmoja hata kwenye viti visivyokuwa na abiria kwa wakati wa ukaguzi huo.
5. Magari kutozwa faini kwa defect yoyote kwenye bodi hata ya rangi tu.
6. Magari kutozwa faini kwa madai kuwa rangi kwenye kadi za magari siyo 100% perfect kama ilivyo kwenye kadi.
7. Gari kutozwa faini kwa tathmini za macho kuhusu matairi (labda yawe mapya!).
8. Nk, nk.
Alimradi kila gari ya asiyekuwa mkomavu wa type za washupavu za raia wa jamhuri ya Twitter, alirambwa 30,000/=.
Lugha yao rasmi: "Basi acha tukuandikie angalau kosa moja."
Katika safari nzima nimeshuhudia vitimbi vyao vingi achilia mbali vya wale wa kwenye railway crossings za Manyoni na Bahi, wenye kuvizia magari yasiyosimama kwenye vivuko hata kama hamna treni inayokuja kwa wakati huo.
Vitimbi vyao hivi ni vyenye kutia mashaka sana, kama kweli hawa waliopaswa kutulinda wana hata uelewa wa kuwa mishahara yao ni kodi kutoka kwa hao ambao wao ndiyo wamewageuza kuwa wahanga wa dhuluma zao hizi. Na au je, ni mwendelezo ule ule tu wenye mlengo wa kumhujumu kipenzi cha watu Mama Samia rais wa JMT, kwa wananchi?
Hivi abiria asiyefunga mkanda au hata furushi la abiria, kwa nini ziwe ni kesi za dereva ambaye mashimo na mabonde yote barabarani ni yake?
Nikadhani uzi huu hautakamilika bila japo kusimama na kuwasalimia rasmi walinzi wetu hawa pale kituoni kwao, wilayani Biharamuro.
Kwa mshangao nikakutana na bango kubwa lenye maandishi haya:
"Karibuni wateja, karibuni sana."
Ama! Kumbe sisi ni wateja!
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂!
Pana umuhimu wa kuona namna ya kukomesha dhuluma hizi.
Ninaandaa uzi husika wenye muarobaini na sera za wazi zenye uwezekano wa kuhitimisha dhuluma zote binafsi hizi.