Watawala haramu wamelitia taifa katika laana ya mauaji. Damu za watu huleta laana katika nchi. Sasa mauaji ya watu umegeuzwa kuwa utamaduni wa watanzania!
Mungu, tunaomba uturehemu, kwa mkono wako wenye ukuu tunaomba utuondolee laana hii ya mauaji kama Taifa, laana ikawaguse tu wauaji na washangiliaji wa mauaji na vizazi vyao. Tunaomba utujalie moyo wa upendo ili watanzania turudi katika upendo wako, tena tukafurahie na kuitamani haki kuliko dhuluma. Tunaomba ukamlinde kila mwenye kuitamani na kuitafuta haki, na utuondolee kwenye uso wa nchi yeye afurahiaye dhuluma na mauaji.