Polisi: Dereva aliyekuwa anaendesha gari akichati na kutoa lugha chafu atiwa mbaroni

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
TAARIFA KWA UMMA
DEREVA ALIYEKUWA ANAENDESHA GARI HUKU AKICHATI, KUTOA
LUGHA CHAFU ATIWA MBARONI​

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia, Sabatho Malima Emmanuel, mwenye umri wa miaka 32 na mkazi wa Buswelu, Wilaya ya Ilemela, ambaye ni dereva wa basi la Kampuni ya Obadia lenye namba za usajili T 870 DVW, aina ya Yutong, linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Nyamongo mkoani Mara kwa kosa la kuendesha chombo cha moto kwa njia ya hatari na kutojali watumiaji wengine wa barabara huku akitumia simu ya mkononi (akichati), kitendo kilichohatarisha maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Dereva huyu amekematwa tarehe 05.09.2026, majira ya saa 6.40 mchana, katika eneo la Isangijo, wilaya ya Magu, barabara ya Mwanza-Musoma, akiwa anatokea Nyamongo kuelekea Mwanza, ambapo alikuwa akiendesha gari hilo huku akichati kwa simu kuanzia maeneo ya Lamadi mkoani Simiyu, kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za Usalama Barabarani na Usafirishaji

Licha ya baadhi ya abiria waliokuwa wameketi kwenye siti za karibu kumuonya na kumtaka aache kitendo hicho kinachohatarisha maisha yao, mtuhumiwa aliwatolea lugha chafu na zenye kubughudhi. Jeshi la Polisi lilichukua hatua za haraka na kumkamata dereva huyo, ambapo tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano na hatua nyingine za kisheria.

Hatua za awali tayari zimechukuliwa ikiwemo kuifungia leseni yake ya udereva kwa kipindi cha miezi sita kuanzia leo tarehe 06.09.2026 na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kukamatwa kwa dereva huyu ni matokeo chanya ya elimu endelevu inayotolewa na Jeshi la Polisi kwa wananchi, hususani abiria kwenye vyombo vya usafiri wa umma, kuwahimiza kupaza sauti na kutoa taarifa dhidi ya madereva wasiozingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.

Jeshi la Polisi linawapongeza abiria hao kwa kutonyamaza kutokana na kitendo kiovu cha dereva huyo cha kuhatarisha maisha yao na ya watu wengine. Aidha, linatoa wito kwa madereva wote kuacha mara moja tabia ya kutumia simu wakati wa kuendesha pamoja na kutoa majibu ya dharau kwa abiria, kwani hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayehatarisha maisha ya wananchi barabarani.

Imetolewa na: -
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza

Soma pia Video: Je, ingekuwa wewe ndo abiria wa hili basi ungechukua uamuzi gani?

1788701571496.png

1788701345682.png

1788701470773.png
 
Attachments

  • 1788701514113.png
    1788701514113.png
    690.8 KB · Views: 10
Tatizo madereva wa kizazi cha yutong Zhongtong Asia star⭐ dragon wana mihemko sana jeshi la usalama barabarani lingeachwa lifanye kazi yake kwa weledi bila kuingiliwa na wanasiasa ajali zingepungua kwa asilimia 95
 
TAARIFA KWA UMMA
DEREVA ALIYEKUWA ANAENDESHA GARI HUKU AKICHATI, KUTOA
LUGHA CHAFU ATIWA MBARONI​

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia, Sabatho Malima Emmanuel, mwenye umri wa miaka 32 na mkazi wa Buswelu, Wilaya ya Ilemela, ambaye ni dereva wa basi la Kampuni ya Obadia lenye namba za usajili T 870 DVW, aina ya Yutong, linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Nyamongo mkoani Mara kwa kosa la kuendesha chombo cha moto kwa njia ya hatari na kutojali watumiaji wengine wa barabara huku akitumia simu ya mkononi (akichati), kitendo kilichohatarisha maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Dereva huyu amekematwa tarehe 05.09.2026, majira ya saa 6.40 mchana, katika eneo la Isangijo, wilaya ya Magu, barabara ya Mwanza-Musoma, akiwa anatokea Nyamongo kuelekea Mwanza, ambapo alikuwa akiendesha gari hilo huku akichati kwa simu kuanzia maeneo ya Lamadi mkoani Simiyu, kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za Usalama Barabarani na Usafirishaji

Licha ya baadhi ya abiria waliokuwa wameketi kwenye siti za karibu kumuonya na kumtaka aache kitendo hicho kinachohatarisha maisha yao, mtuhumiwa aliwatolea lugha chafu na zenye kubughudhi. Jeshi la Polisi lilichukua hatua za haraka na kumkamata dereva huyo, ambapo tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano na hatua nyingine za kisheria.

Hatua za awali tayari zimechukuliwa ikiwemo kuifungia leseni yake ya udereva kwa kipindi cha miezi sita kuanzia leo tarehe 06.09.2026 na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kukamatwa kwa dereva huyu ni matokeo chanya ya elimu endelevu inayotolewa na Jeshi la Polisi kwa wananchi, hususani abiria kwenye vyombo vya usafiri wa umma, kuwahimiza kupaza sauti na kutoa taarifa dhidi ya madereva wasiozingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.

Jeshi la Polisi linawapongeza abiria hao kwa kutonyamaza kutokana na kitendo kiovu cha dereva huyo cha kuhatarisha maisha yao na ya watu wengine. Aidha, linatoa wito kwa madereva wote kuacha mara moja tabia ya kutumia simu wakati wa kuendesha pamoja na kutoa majibu ya dharau kwa abiria, kwani hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayehatarisha maisha ya wananchi barabarani.

Imetolewa na: -
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza

Soma pia Video: Je, ingekuwa wewe ndo abiria wa hili basi ungechukua uamuzi gani?

Ngoja akasugue benchi miezi sita ataiona miaka 6
 
Halafu mtoto mdogo tu alifikiri kushika strerling ya basi ndiyo amekuwa kila kitu. Ukitoka kwenye ujinga na umaskini ni mzigo kwa jamii
 
Dereva kafanya tukio siku hiyo na kukamatwa siju hiyohiyo lakini watekaji wa emanuel nchimbi,hamphrey polepole,dioniz,mzee kibao,tundulisu,soka,ben saanae hawajapatikxna hadi leo pamoja na kwamba imepita zaidi ya miaka mitatu.
 
Back
Top Bottom