KERO Polisi fanyeni usaili wenu kikanda, kutoa watu mikoa tofauti kufanyia usaili Dar ni usumbufu mkubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
IMG_3285.jpeg

Gaweni kikanda Tanzania bara ni pakubwa sana, mnategemea mtu kutoka Kagera aje Dar kwenye usaili? Mtu kutoka Mbeya huko aje Dar kwenye usaili? Tumieni hekima na busara gaweni kikanda wekeni usawa na haki, mpate watu sahihi.
 
View attachment 3049882
Gaweni kikanda Tanzania bara ni pakubwa sana , mnategemea mtu kutoka Kagera aje Dar kwenye usaili ? Mtu kutoka Mbeya huko aje Dar kwenye usaili ? Tumieni hekima na busara msiwe kama watu mazuzu na wasio na akili gaweni kikanda wekeni usawa na haki , mpate watu sahihi.
Acha kulalamika mbona ajira portal watu wanatoka mbali
 
View attachment 3049882
Gaweni kikanda Tanzania bara ni pakubwa sana , mnategemea mtu kutoka Kagera aje Dar kwenye usaili ? Mtu kutoka Mbeya huko aje Dar kwenye usaili ? Tumieni hekima na busara msiwe kama watu mazuzu na wasio na akili gaweni kikanda wekeni usawa na haki , mpate watu sahihi.
Ni jambo la kusikitisha kuona nafasi za polisi zinagawiwa kwa watoto wa watu wenye uwezo wa fedha na walio karibu na Dar, Pemba na Unguja! Kwa watoto walio mbali na miji hiyo na wazazi wasio na uwezo ni vigumu kupata nafasi hizo!

IGP Wambura mwenyewe asingekuwa katika nafasi hiyo kama usaili wake ungefanyika kwa namna hii kwani asingeweza kusafiri kutoka Kanda ya Ziwa hadi Kurasini Dar.

Hali hiyo pia ingewakumba wengi wa maofisa waandamizi waliopo hivi sasa kwa sababu wengi wanatoka familia za kawaida.

Kwa nini usaili wa awali usingefanyika katika mikoa yao? Watakaofaulu usaili wa awali wapelekwe chuoni Kurasini kwa usaili zaidi na gharama zibebwe na serikali. Hii ingewasaidia sana watoto wanaotoka katika familia za kawaida!

Waziri wa Mambo ya Ndani fikiria kwa makini jambo hili. Wapemba na Waunguja watafanya usaili kwao iweje na kwa sababu zipi Watanganyika wote waende Dar?
 
View attachment 3049882
Gaweni kikanda Tanzania bara ni pakubwa sana, mnategemea mtu kutoka Kagera aje Dar kwenye usaili? Mtu kutoka Mbeya huko aje Dar kwenye usaili? Tumieni hekima na busara gaweni kikanda wekeni usawa na haki, mpate watu sahihi.
Nimeshangaa sana hii kitu visiwan wameweka maeneo ya usaili pemba na unguja ila tanganyika wameweka dar tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
View attachment 3049882
Gaweni kikanda Tanzania bara ni pakubwa sana, mnategemea mtu kutoka Kagera aje Dar kwenye usaili? Mtu kutoka Mbeya huko aje Dar kwenye usaili? Tumieni hekima na busara gaweni kikanda wekeni usawa na haki, mpate watu sahihi.
Hawa watu akili zao sijui wanazitumia kuwaza nini! Ukumbuke hawatapewa nauli,chakula Wala malazi.
 
Hivi ajira za polisi hazipitii ajira portal? Kama wamepewa mamlaka ya kuajiri wenyewe nafikiri wangeajiri kikanda jeshi lingepata mchanganyiko mzuri wa watumishi wake wenye sifa za kufanya kazi
 
Ni jambo la kusikitisha kuona nafasi za polisi zinagawiwa kwa watoto wa watu wenye uwezo wa fedha na walio karibu na Dar, Pemba na Unguja! Kwa watoto walio mbali na miji hiyo na wazazi wasio na uwezo ni vigumu kupata nafasi hizo!

IGP Wambura mwenyewe asingekuwa katika nafasi hiyo kama usaili wake ungefanyika kwa namna hii kwani asingeweza kusafiri kutoka Kanda ya Ziwa hadi Kurasini Dar.

Hali hiyo pia ingewakumba wengi wa maofisa waandamizi waliopo hivi sasa kwa sababu wengi wanatoka familia za kawaida.

Kwa nini usaili wa awali usingefanyika katika mikoa yao? Watakaofaulu usaili wa awali wapelekwe chuoni Kurasini kwa usaili zaidi na gharama zibebwe na serikali. Hii ingewasaidia sana watoto wanaotoka katika familia za kawaida!

Waziri wa Mambo ya Ndani fikiria kwa makini jambo hili. Wapemba na Waunguja watafanya usaili kwao iweje na kwa sababu zipi Watanganyika wote waende Dar?
Hoja zako Zina mashiko, the same succeeded.

Hii naona kama ni 'sabotaging attack techniques' dhidi ya watoto wa Watu wenye kipato kidogo ili wasipate nafasi ya kuhudhuria usaili huo na ili kuwapunguzia ushindani 'watu wao' ambao Jeshi la Polisi limepanga kuwapatia ajira.
Children of the low income earners technically have been sabotaged by the Police Forces in attending the planned recruitment process.
 
Na pia usaili gani unafanyika wiki mbili? Ni usaili wa namna gani huo wanaenda kufanya kuzingatia changamoto zote hizo haswa gharama??
 
Ni njama za makusudi kuwaengua watoto wa familia za kawaida!
 
Jeshi la polisi ni takataka kabisa(toilet papers)yaani mtanganyika atoke kakonko Kuja kufanya usaili Dar? Wakati huo mpemba anafanyiwa upembani kwao na muunguja anafanyiwa usaili unguja.Hili jeshi la ccm linatakiwa kufumuliwa kabisa ili kuondoa ukiritimba wake
 
Kuna mambo ukiyaona unajiuliza hawa walitumia makalio kufikiria!! Mtu yupo tarime,kagera huko, aje dar, naul, malazi chakula juu yake, kwa wazazi wasiojiweza huyu atafikaje huku.
 
Maan
Ni njama za makusudi kuwaengua watoto wa familia za kawaida

Ni njama za makusudi kuwaengua watoto wa familia za kawaida!
Kwanza hawa polisi saili zao zikoje?? Hizo week mbili watu wanakaa camp maana kiukweli ni kuwa tesa watu, mtu anaweza kujikusanya kutoka Kagera huko akaenda kwenye usaili maskini ya mungu na asipite..Haya mambo asee sio poa
 
Jeshi la polisi ni takataka kabisa(toilet papers)yaani mtanganyika atoke kakonko Kuja kufanya usaili Dar? Wakati huo mpemba anafanyiwa upembani kwao na muunguja anafanyiwa usaili unguja.Hili jeshi la ccm linatakiwa kufumuliwa kabisa ili kuondoa ukiritimba wake
Linatakiwa kuvunjwa lote kabisa na kisha liundwe Tena lingine kwa sababu hili lililopo tayari limepoteza kabisa Uhalali wa kuwa Jeshi la Polisi ktk nchi yoyote ile hapa duniani.
 
Usaili wa wiki mbili ni usaili wa namna gani huo??
 
kinachoshangaza ni usahili kufanyika ndani ya wiki mbili! bora hata wangetaja kila siku iwe na idadi yake na majina yake
 
Back
Top Bottom