KERO Polisi fanyeni usaili wenu kikanda, kutoa watu mikoa tofauti kufanyia usaili Dar ni usumbufu mkubwa

KERO Polisi fanyeni usaili wenu kikanda, kutoa watu mikoa tofauti kufanyia usaili Dar ni usumbufu mkubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Jamani kwani usaili wa polisi mikoani mfano iringa ni ofisi gani za kuripoti
 
Ni jambo la kusikitisha kuona nafasi za polisi zinagawiwa kwa watoto wa watu wenye uwezo wa fedha na walio karibu na Dar, Pemba na Unguja! Kwa watoto walio mbali na miji hiyo na wazazi wasio na uwezo ni vigumu kupata nafasi hizo!

IGP Wambura mwenyewe asingekuwa katika nafasi hiyo kama usaili wake ungefanyika kwa namna hii kwani asingeweza kusafiri kutoka Kanda ya Ziwa hadi Kurasini Dar.

Hali hiyo pia ingewakumba wengi wa maofisa waandamizi waliopo hivi sasa kwa sababu wengi wanatoka familia za kawaida.

Kwa nini usaili wa awali usingefanyika katika mikoa yao? Watakaofaulu usaili wa awali wapelekwe chuoni Kurasini kwa usaili zaidi na gharama zibebwe na serikali. Hii ingewasaidia sana watoto wanaotoka katika familia za kawaida!

Waziri wa Mambo ya Ndani fikiria kwa makini jambo hili. Wapemba na Waunguja watafanya usaili kwao iweje na kwa sababu zipi Watanganyika wote waende Dar?
Tatizo NI WASOMI washauri kuwa Kada badala ya competences
 
Duuh nmesoma Hilo tangazo hapo juu, naona wameandika kuwa six na four usaili watafanya mikoa walioichagua, Sasa mikoa walioichagua wapi? Makao makuu ya mikoa au wapi?...Poleni sana.
 
Back
Top Bottom