Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jeshi la Polisi limekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai gari lililoegeshwa Kituo cha Polisi Gogoni limehusika na tukio la utekaji wa Abdul Omary Nondo katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli leo alfajiri.
Pia, Soma: Zitto: Tumepata Taarifa Nondo yuko Kituo cha polisi Gogoni, Tumefika tumekuta gari inabadilishwa Plate namba
Kwa mujibu wa Polisi, gari hilo ni la Serikali na limekuwa likiegeshwa kituoni hapo tangu Novemba 29, 2024. Leo mchana, lilichukuliwa na dereva kwenda kuoshwa kwa maandalizi ya kazi za kesho. Aidha, mashuhuda wanasema gari lililotumika katika tukio halikuwa na ngao, tofauti na gari hilo la Gogoni.