A
Anonymous
Guest
Habari Wanajamvi,
Tunapoelekea kwenye suala la Uchaguzi nchi imeendelea kuchafuka kweli, matukio ya utekaji na kupotea watu yanazidi kuongezeka. Baadhi ya Wananchi hususan wafuasi wa Vyama vya Upinzani wamekuwa wakishutumu Vyombo vya Dola kwa kutumia Polisi kuhusika moja kwa moja na Utekaji huu mathalani utekaji wa hivi karibuni wa Mzee Ali Mohammed Kibao.
Soma: TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Matukio haya mengi sana hata ya wale Vijana wa Kariakoo waliokuwa wanapotea na kupatikana wamefariki huwa yaanza na stori kuwa mtu alikuja kuchukuliwa na Watu waliojitambulisha kama ni Polisi. Baada ya siku kadhaa atatafutwa na watu wake na kutoonekana na baadaye anaweza kupatikana katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwenye moja ya hospitali.
Soma: Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati
Kutokana na hili, kuna uwezekano Jeshi la Polisi halihusiki na hivi vitu au kuna uwezekana kuna kitengo cha watu wachache katika Polisi wanafanya haya na hivyo kuchafua Jeshi letu lenye kulinda amani ya nchi na Wananchi.
Katika kujisafisha ningeshauri Jeshi la Polisi liweke mfumo wa kumsaidia Mwananchi wakati anapokamatwa aweze kutambua mtu anayemkamata. Mfumo huu unaweza kuwa kama ule wa utambuzi wa Mawakili ambapo mtu ukiingiza namba au jina la Wakili unapata taarifa zake.
Mfano namna ulivyo mfumo wa kuangalia Mawakili: https://ewakili.judiciary.go.tz/#/ewakili/home
Polisi katika tovuti yao wanaweza kuweka mfumo ambapo mtu akikamatwa na Polisi kujitambulisha, Mwananchi anaweza kuweka Force Number ya Polisi au Jina lake kamili na akapata taarifa zake kama cheo chake, kitengo alichopo na Kituo chake cha Kazi na kama ni Polisi ‘active’
Nasema hivi kwani kuna uwezekano mkubwa sana kuna watu wamechukuliwa na Polisi feki walioghushi Kitambulisho cha Polisi au taarifa nyingine za Polisi na ubaya ni kwamba Polisi wetu wamekuwa wakienda kukamata watu mara nyingi wakiwa na nguo za kiraia, jambo linalowapa urahisi hata wa halifu kujifanya Polisi.
Hii itaasaidia sana watu kujua mtu kama sio Polisi na kukataa kwenda naye lakini pia kama ni Polisi ni rahisi mtu akichukuliwa kutuma taarifa hizi kwa ndugu, jamaa au mtu wa karibu ili kuwajulisha amechukuliwa na Polisi gani na hata akipatwa na kitu basi inakuwa rahisi kujua pa kuanzia.
Polisi wanaweza kuwa na mfumo huu kama waliweza kuweka mfumo wa watu kuangalia madeni yao ya kwenye magari au lesini hawashindwi kuweka huu mfumo wa watu kuhakiki taarifa za Polisi. Jeshi letu sikivu ni vema kushughulikia hili na kujiepusha na kashfa hizi