Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Askari polisi jamii Kata ya Sakina - Arusha ambaye alikuwa pia dereva toyo kwa jina la Goodluck William afariki dunia baada ya kuchapwa viboko 70 kama adhabu aliyopewa na wazee kutokana na mila za Kimasai sababu ikisemekana ni kutelekeza familia yake, ambapo familia yake hiyo aliiacha Monduli, Arusha.
Taarifa ya kifo chake zilisambaa siku ya Jumatatu Tukio Jumatatu tarehe 8/7/2024 baada ya kuchukuliwa na ndugu zake siku ya Jumapili 7/7/2024 kupelekwa Monduli.
Baadhi ya polisi jamii wenzake walimuelezea marehemu kama kijana mpole, ambaye alikuwa hataki kuonewa au kuonea na amefanya kazi kwa miaka 15 na hata ukimtuma mtu kwenda kumchukua mharifu alikuwa anaenda na kumchukua mharifu bila kumjeruhi wala kumnyanyasa.
Na yeye pia alikuwa msaada mkubwa moto ulivyotokea katika hata hivyo, katika kusaidia kuuzima ili usilete madhara makubwa.
Global TV.