PreGE2025 Polisi Kahama wadaiwa kazuia maandalizi ya Mkutano wa CHADEMA, wadai eneo limebadilishwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baada ya mvutano kati ya Polisi na CHADEMA, hatimaye imekubalika kuwa mkutano wa chama utafanyika katika eneo lililokusudiwa. Awali, Polisi walifika na kuzuia maandalizi yaliyokuwa yakiendelea kwa maelezo kwamba eneo hilo limebadilishwa, licha ya kuwa jukwaa na mfumo wa sauti (PA System) vilikuwa tayari vimefungwa. Maamuzi ya kuruhusu mkutano huo kufanyika yalifikiwa baada ya mabishano kati ya viongozi wa chama, Polisi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama.

Capture.PNG

Capture.PNG
Awali ilinadaiwa kuwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kahama leo tarehe 17 Mei 2025 limeingilia maandalizi ya mkutano wa CHADEMA uliotarajiwa kufanyika jioni ya leo, likizuia shughuli zote zilizokuwa zinaendelea katika eneo la mkutano.

1747476522911.png
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gwamaka Mbughi kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Polisi walifika katika eneo ambalo maandalizi ya mkutano yalikuwa yamekamilika, likiwemo jukwaa na mfumo wa sauti (PA System), na kutoa agizo la kusitisha shughuli hizo kwa maelezo kuwa eneo hilo limebadilishwa.

1747476579465.png

L.PNG

​
 
Polisi wanatumika kiboya sana wakitoka hapo wanaenda kulala kwenye viboksi vya mabati kama njiwa.
 
Polisi na boss wao anayewatuma hadi uchaguzi huu kama utakuwepo uishe watakuwa na vidonda vya tumbo na shinikizo la damu.

Kweli acheni wamuite Lissu mropokaji, maana kwa kuropoka kwake Sultan kachoka anaandaa drama ya vidampa wake kutoka CHADEMA, na sasa polisi na bosi wao wa Kizimkazi wako busy na kivuli cha Lissu.
NO REFORM NO ELECTION inawatesa
 
Back
Top Bottom