Polisi wasio na weledi ndio wanakimbilia kutumia silaha, Polisi majambazi ndio wanaua watu na kuwabatiza ujambazi, Polisi wa mambosasa mwenye fremu za maduka 100 mabwepande ndio deal likibuma wanakuondosha usijewataja.
Kumbuka mnaowaua wana wategemezi wao ambao wataathirika maisha bila hatia, kumbuka laana mnayoitengeneza mpaka kizazi chenu cha tatu itawatafuna hata mkiwa kaburini.
Mh. Samiah badilisha uongozi wa polisi makao makuu, mpe mtu ambaye ni kweli analipenda jeshi na amefanya utafiti mpaka amepata PhD ya kazi za Polisi zinavyotakiwa kuendeshwa atarudisha heshima ya taasisi hii ambayo wananchi wanaichekea mdomoni moyoni wanalia, wanaiogopa hawaipendi, wanahofu nayo na wala hawaiheshimu.
Wapo polisi wamewekeza kwenye uhalifu wanafanya uhalifu ndio kitega uchumi wanashiriki moja kwa moja ujambazi nakisha rais ukiwalaumu hawafanyi kazi wanatafuta wa kuwatoa kafara wakuridhishe. Inauma sana.