Polisi kanda ya Dar kuanza kutoa zawadi (Reward For Justice) kwa raia wema wanaofichua uhalifu

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari za muda huu waungwana wa jamiiforums.



JUNE 23, 2021: Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya DSM, ACP Muliro Jumanne Muliro ametangaza rasmi kuwa Mtu yeyote atakaetoa taarifa sahihi zitakazowezesha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM kumkamata Mhalifu akiwa na silaha mfano; bunduki atatoa zawadi papohapo ya Tsh. Milioni mbili na kuhakikisha siri za mtoa taaarifa zinatunzwa kwa kiwango cha juu na bila kuathiri mazingira ya usalama wake, zawadi hizo zitaanza kutolewa bila kuzungushwa ilimradi vigezo vilivyotajwa vizingatiwe.



USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
ANGALIZO: Ukiona jambo lina manufaa kwa Tanzania, toa taarifa kwa viongozi wako ili liwe na msaada wa jamii nzima inayokuzunguka.
 
Dah bora fursa ziongezeke maana kuna janga la ukosefu wa ajira. Ila nashauri iwe nchi nzima ili na sisi wa mikoani tufaidi hii fursa.
 
Na vip kama uhalifu unawahusu hao polisi wenyewe natoa wapi taarifa yangu? maana kuna polisi pia ni wahalifu ila wamejificha kwenye vazi la upolisi ili kutekeleza uharifu wao kiurahisi zaidi
 
Na vip kama uhalifu unawahusu hao polisi wenyewe natoa wapi taarifa yangu? maana kuna polisi pia ni wahalifu ila wamejificha kwenye vazi la upolisi ili kutekeleza uharifu wao kiurahisi zaidi
Nenda kwa Polisi mwenye cheo cha juu kuwazidi utoe taarifa
 
Muwe makini tu, Hao polisi sio viumbe wa kujichanganya nao sana...Wakianza tu ma zile mambo zao za kukuhitaji kwene uchunguzi usije kushangaa umepikwa kwenye tukio hilo
 

Siku moja kuna jamaa x alikwenda kumchoma mtu fulani lakini yule mtu alikuwa na mkwanja na sapport ya wakubwa vitengo mbali mbali(africa ya rushwa).alicho fanya baada ya kugundua kuwa kachomwa haka toa mpunga mrefu ili kutoka.
Kilicho fata kwa jamaa x yeye ndio alikula kesi ya bunduki na akafa kioro.

Kazi ya polisi ni kulinda jamii na kujua yote.

Zawadi zitakuja kuleta matatizo.kama uamini fanya kwa watu
 
Alieliweza hili ni Mrema pekeyake.. Ilikuwa haina longolongo na anakupatia mwenyewe direct, wengine wote waliofuatia michakato yao ilijaa walakini iliyopelekea watoa taarifa kuumizwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…