jamesmwakalinga
Member
- Oct 17, 2024
- 6
- 7
Jiehi la plisi mkoani Kilimanjaro,linashilikia simu za kiganjani za mfanyabiashara maarufu mjini moshi(jia tunalo)akihusishwa na tukio la kumwagiwa kimiminika kinachoaminika kuwa ni tindikali kada wa ccm,Idrisa Makishe.
Makishe(38)mkazi wa Bomambuzi Manispaa ya Moshi,yupo kitandani akipambania uhai wake baada ya watu wasiojulikana kummwagia kimiminika kinachoaminika kuwa ni tindikali.
Makishe ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi(CCM) na mwendeshaji wa Bodaboda alikumbwa na mkasa huo septemba 20 mwaka huu saa 2 usiku baada ya mtu mmoja kutumia mbinu ya abiria kumkodisha kutoka kwenye kijiwe chake kilichopo mtaa wa uswahilini kuelekea Njoro Relini.
Kwa mujibu wa Taarifa ya jeshi la polisi kupitia kamanda wa mkoa wa Kilimanjaro(SACP),Simon Maigwa,mtu huyo baada ya kuondoka na Makishe na wakiwa njiani alimuomba asimame ili amchukue mwenzake na dakika chache mtu huyo alitokea na kumwagia kimiminika hicho.
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi mjini moshi,zinadai kuwa,siku chache baada ya tukio hilo,polisi walimuita kwa mahojiano mfanyabiashara huyo na baadaye kushikilia simu zake.
Kushikiliwa kwa simu za mfanyabiashara huyo anayemiliki pia vituo vya mafuta pamoja na mabasi ya abiria,kulitokana na kuvuja kwa taarifa za yeye kuhusishwa na tukio hilo linatojwa kuwa linatokana na misingi ya kisiasa.
Hadi sasa ukiondoa taarifa za kushikiliwa kwa simu za mfanyabiashara huyo ambaye pia ni kada wa CCM, hakuna taarifa huru za kukamatwa ama kuhojiwa kwa watu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo.
Baada ya tukio hilo watu hao walimpora pikipiki yake aina ya Sonorai yenye namba za usajili MC854 DCB na kuondoka nayo na kumuacha Makishe akipambana kusaka msaada na baadae kukimbizwa Hopsital ya rufaa ya mkoa,Mawenzi kabla ya kuhamishiwa Hospital ya rufaa ya kanda,KCMC kwa matibabu zaidi.
Taarifa ya RPC Maigwa ikahitimisha kwa kuomba ushirikiano kutoka kwa wananchi ili kufanikisha waharifu hao kuweza kutiwa mbaroni na kufikishwa kwenye mkono wa sheria japo mpaka tunachapisha habari hii hakuna hata mmoja aliyekamatwa na kuhojiwa juu ya tukio hilo.
Matukio haya ya watu kumwagiwa tindikali yamewatia hofu wakazi wa mji wa moshi na baadhi wanahoji wako wapi watesi wa Tariq na Makishe,nani anawalipa watu hawa na kwa sabubu gani ?
Wanaomfahamu Makishe wanadai tukio hilo linahusishwa na misingi ya kisiasa wakidai Makishe na makada wenzake wamekuwa wakosoaji wakubwa kwa viongozi wa ccm ambao wamekuwa hawatekelezi majukumu yao ndani ya chama.
Wanadai Makishe ameumizwa na ukosoaji wake huku wakimnyooshea kidole mfanyabiashara mmoja mwenye ukwasi mkubwa na ambaye pia ni kada wa chama cha mapunduzi(ccm)wakimhusisha na tukio hilo.
Hata hivyo Raia Mwema limeshindwa kuweka jina la mfanyabiashara huyo kwani muda wote amekuwa akipigiwa simu bila mafanikio licha ya video fupi inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimtaja moja kwa moja.
MBUNGE PRISCUS TARIM0 ALAANI
Siku moja baada ya tukio hilo kutokea,mbunge wa jimbo la moshi mjini,Priscus Tarimo(ccm)alilaani tukio hilo huku akimtakia uponyaji wa haraka wakati vyombo vya uchunguxzi vikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
“Ninalaani kwa nguvu zote tukio hili,Idrisa Makishe jana jioni (septemba 20)amekodiwa kutoka kituo cha bodaboda cha Kizota Kata ya Bondeni, kumpeleka abiria Njoro na kwa bahati mbaya abiria wake na mtu mwingine aliyekuwa anasubiri kwenye eneo alilotaka kupelekwa abiria kwenye Kata ya Njoro”
“Walimvamia, kumpiga na nyundo kichwani, kumwagia kimiminika kinachoaminika kuwa tindikali usoni na sehemu nyingine za mwili na kisha kuondoka na pikipiki yake kuu kuu”
“Wahusika walitaka lionekane kama tukio la unyang’anyi au uporaji lakini kwa muonekano wa awali kuna mazingira ya udhalimu wa kisiasa”;aliandika Priscus kupitia ukurasa wake wa facebook na kuongeza.
“Ninamtakia uponyaji wa haraka na wa uhakika ndugu yetu Idrisa Makishe wakati tukisubiri taarifa zaidi kutoka kwenye vyombo husika”alihitimisha Priscus.
Taarifa hii imekusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari likiwamo Gazeti la Raia Mwema toleo la jumatano oktoba 23,2024