Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikiliwa watuhumiwa 18, akiwamo Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Felius Kinimi, wakituhumiwa kufanya mikusanyiko iliyo kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao leo Septemba 6, 2025, akisema wamekamatwa eneo la Sambarai Kibosho, wilayani Moshi.
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikiliwa watuhumiwa 18, akiwamo Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana Taifa, Chadema kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko iliyo kinyume cha sheria sambamba na kupanga njama za kuhamasisha vurugu na kuhatarisha amani na usalama nchini," imeeleza taarifa ya Jeshi la Polisi.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, limekuwa likiwafuatilia sambamba na kukusanya ushahidi na leo Septemba 6, walipokuwa wanakwenda kutekeleza vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria ndipo likawatia nguvuni.
Jeshi hilo limetoa onyo kwa yeyote anayepanga njama za kuhamasisha na kufanya vurugu ili kuhatarisha amani, utulivu na usalama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu na baada ya uchaguzi halitasita kuwakamata ili sheria ichukue mkondo wake.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Samwel Welwel imesema msafara wa viongozi wa Bavicha Taifa na kanda hiyo ukiwa njiani kuelekea nyumbani kwa kina Deusdedith Soka kama sehemu ya kuenzi mashujaa wa chama hicho polisi walizuia msafara wao.
Soka alitoweka takribani mwaka mmoja umepita na hajawahi kuonekana.
Chanzo: Mwananchi