Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
KILIMANJARO INAKWENDA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI
Jeshi la polisi mkoani kilimanjaro,limeweka mkakati wa kupunguza ajali za barabarani ambazo licha ya kupoteza maisha ya watu na wengine kuachwa na ulemavu wa kudumu,zimekuwa chanzo cha kupoteza nguvu kazi na uharibifu wa mali.
Mkakati huo umewekwa wazi na Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Lazaro Mwanyasi Mkuu wa Polisi Jamii mkoani Kilimanjaro wakati akifunga mafunzo ya madereva wa Bajaji na Pikipiki (Bodaboda) 65 waliohitimu mafunzo hayo Juni 8, 2024 na kupatiwa cheti cha awali cha Udereva.
Mwanyasi amesema Kilimanjaro inakwenda kumaliza tatizo la ajali barabarani kwani wahanga wakubwa wa ajali ni Bodaboda na bajaji ambao wengi wao wamejitolea kupata elimu ya sheria za usalama barabarani na udereva salama kwa watumia barabara wote.
Aidha, amewataka madereva hao kujiwekezea kipato katika Saccos ya Madereva iliyoanzishwa ili kukuza kipato na kuacha tabia za kujiingiza katika matukio ya kihalifu kama kusafirisha dawa za Kulevya na nyara za Serikali.
Katika upande wake Mkurugenzi wa Huruma Driving school Mr Gilbert Mngoni ambao ndio wafadhili wa mafunzo hayo wakishirikiana na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani mkoani Kilimanjaro amesema jumla ya vijana 465 walijitokeza kupata mafunzo hayo na waliokidhi vigezo vya kuhitimu ni vijana 65 ambao wametunukiwa vyeti.
Habari hii imeandaliwa na Mwandishi wa Dawati la Habari Polisi Kilimanjaro.