Polisi kitengo cha loss report Arusha hili limekaaje?

Ni kweli wala hajakosea...

Wana computer lakini hazina internet wala network...
 
Una ushahidi juu ya hilo la mwisho?

kamwamu

JF-Expert Member​

May 18, 2014 3,075 2,000

Cyber crime utafutaji simu ni dili zuri sana kwao. Huzifuatilia simu na pindi wakizipata humbandika mtu kesi ya mauaji. Kujinasua hapo ni mamlioni ya shilingi. Mpotezaji hudaiwa, anaepatikana nayo ni balaa.

Quote Reply
Report
 

Attachments

  • 1614955958788.gif
    42 bytes · Views: 1
Naona kuna wengine wanasema iko online hebu tuelekezane wakuu jinsi ya kuipata.
Ingia website ya police .www.policetz.com kilaa kitu kipo hapo,unaandika report yako then upewa control number chap kwa mpesa au Tigo pesa,unamprint karatasi then unaenda polisi waakiki!kuna dawati police unawapa number ya muamalaa wanakungongea mihuri Ina kuwa umemaliza.au stationary nyingi siku hizi wanahizo hudama

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
mkuu punguza chai
Jaribu hata kutembea mahakaman uone ni jins gan kesi za mauaji zinavyo endeshwa kesi ya mauaji siyo rahisi kumsingizia mtu labda ungesema kesi za wizi, mauaji inatakiwa kuwe na ushahidi wa kutosha siyo kumshika mtu na simu tu
 
Hivi huwa kina kitengo cha loss report, au kitu hiki huwa kinafanywa na polisi yoyote anayehusika kama ilivyo katika kukamata wahalifu?
Siyo polisi yeyote, ni mtu yeyote anayewajibika kwa vitu vidogo vidogo kama loss report
 
sio kweli haipiti ni mpaka uende polisi baada ya kulipia ile control number kule ukimaliza ndio utaweza kuiona online na kuidownload ..
Mtandao ukiwa hovyo utaenda kwa ocs lkn kawaida ukitumia nida hakuna sababu ya kwenda polisi. Kama hujui omba ufundishwe wewe. Leo nimejaza loss report zaidi ya 10 kwa nida, sijaenda kituoni
 
huwezi kuprint mpaka uilipie na uende kituoni kuiverify na kuipitisha ndio utaweza ku view na kuishusha
Ukitumia nida, unalipia hela ya serikali 500 tu. Huna haja ya kwenda kituoni
 
Mkuu jihudumie kuepuka zengwe lolote. Unaogopa nini kujaribu?
 
Line za sim, wallet na mali nyingine sawa utapata loss report bila kwenda polisi, lakini ikiwa iliyopotea ni simu ya mkononi, loss report yake huipati online aisee inakataa
Ha ha ha loss report ya simu? Halafu unaenda kwa nani akupe simu hiyo?

Mali zilizopotea ambazo unahitaji kuzirejesha, utadaiwa loss report. Ipate kwa kujihudumia kupitia Nyumbani

Mali ambazo hakuna mamlaka ya kukurejeshea, unajaza loss report kwa tahadhari. Isitumike ukawajibika wewe. Vyote unapata kupitia link hiyo.

Kama unataka kuitafta mali mfano simu, utalazimika kufungua kesi ili sasa ipate, rb, ir na mpelelezaji. Hapa kuna mchakato mrefu, makampuni ya simu ushirikiano wao ni mbovu kwa madai ya kulinda siri za wateja.
 
Loss report ya kupotea kwa simu? Yaani ulijaza IMEI na ukapata loss report online moja kwa moja bila kwenda polisi?
Inawezekana. Loss report hata usipojaza details kwa usahihi, utaipata tu sema haitokusaidia maana haieleweki
 
Hongera kwa kuuliza na kujijibu mwenyewe mkuu. Inaitwa taarifa ya upotevu, namna gani utaitumia hiyo taarifa ni juu yako mwenyewe.
 
Mtu asipojua kitu ndo anakuwa na matatizo?
Aisee
 
huwezi kuprint mpaka uilipie na uende kituoni kuiverify na kuipitisha ndio utaweza ku view na kuishusha
Inategemea na kitu ulichopoteza mzee kama ni Simcards, Wallets au Card za Bank haina haja ya kwenda Huko kituoni una print tu baada ya kulipia iyo 500, Naongea ivi mana nimefanya iyo process jana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…