OSOKONI
"Heri nusu shari kuliko................"
Hakuna muujiza wowote uliofanywa wa kumuacha hai Dr Ulimboka,zaidi ya Mungu.Hakuna namna yoyote ile ambayo ilimfanya Dr.abaki hai hadi asubuhi ilie kwa mateso yote yale,pamoja na bleeding yote ile.Mungu alipenda huyu jamaa awe hai ili atufunulie yale yaliyo nyuma ya pazia.
Kwa malengo hayo dr. aliwageuka watanzania Mungu hatamsamehe kwa hilo kwani anampango nae.Na hata dr akiwasaliti watz bado Mungu atatupatia mtu mwingine,
ijapokua najua dr. hatakua salama tena kwani hao watesi wake wakimaliza kujiosha, kuna siku watamrudi tu,ili kujihakikishia usalama wao,kwani wanajua kuna siku anaweza kuwageuka vilevile.
Anahitaji kuwa na moyo wa chuma.Ijapokua kwa upande wangu ,dr. alishaaeleza yake siku ile alipokua "mautiuti"kwani pale ndio ukweli ulipojifunua,akija kuongea leo habari yake itakua imekua edited ,kidogo na haitakua sahihi sana kama ile ya siku ya kwanza.Kwa upande wangu taarifa ya kwanza ilikua sahihi ndio maana unamuona Kova alivyokua akitapatapa kama kuku wa mdondo,Mpaka leo bado anahangaika kuweka mambo sawa kwani,kila akiedit ,anaona taarifa bado haikai vizuri.
Mwanahalisi ndio alimalizia kabisa.Kwa watu walio Telecom wataona kabisa ule mtiririko wa Mwanahalisi namna alivyofuatilia zile taarifa kwenye systems unaonyesha waziwazi wahusika.Sihitaji kabisa kusikiliza hata hizo pelepete za Kova.Wenye muda wa kuchezea waende kumsikiliza.Napia hao wanaoenda kumsikiliza nna Imani ni wale wanaofuata zile bahasha za kaki.