Jee ni kweli wadau kuwa maandamano yatokeapo hata yanapokuwa yamefuata sheria polisi huwa wanalianzisha ili kutokee mchanganyiko na wao waingilie kati na kutengeneza fursa ya kipato ndani ya fujo hizo?
Habari hizo baada ya kuzipata na kushangaa nami nikashangawa kuwa ULIKUWA HUJUI CHAKAZA?
Jee nyie wana JF mnalijua hilo? Kwamba mbinu inayotumika ni kujipanga kwanza, kisha amri ya kutawanyika na ghafla mabomu kwenye zile exits zote ambazo ndio zingetumika kutawanyika.
Baada ya hapo ni kipigo, uporaji wa simu na fedha.
Tetesi hizo zinasema baada ya shughuli hiyo sio ajabu kumkuta mtu na simu kumi na fedha ya kutosha.
Jee mnalijua hilo?